BILA Uvumilivu Utaacha Kila Siku, Kuwa Makini Katika hili:;
on
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Ukiwa mtu wa kuangalia mambo kwa juu juu basi kila kitu kwako kitakuwa
kigumu. Kusoma unaweza kuona ni kugumu, kufanya kazi kugumu, hata
kusubiri mshahara unaweza kuona ni kugumu.
Urahisi kwako unaweza kuwa katika kutumia pesa, pengine na kula tu. Ila
watu waerevu na wenye uvumilivu kwako kila kitu kinaweza kuwa tofauti
na wewe.
1. Unachoona kigumu kwao wanahisi si ugumu bali ni changamoto za
kuzidisha jitihada na umakini tu. Kwenye mapenzi pia hali haiko tofauti
sana. Wale wanao achana kila siku si kama ndiyo wanakosewa sana kuliko
wale ambao hawaachani, hapana. Suala ni lile lile tu.
2. Wakati wengine wakiona tofauti zao ni kama changamoto za kusomana
tabia na kuamua kuishi kutokana na kila mmoja kumjua mwenzake. Wenzao
wanaona suluhisho la yote ni kila mmoja kuwa na maisha yake. Suala la
uvumilivu kwao hamna.
3. Hakuna mapenzi duniani yanayoweza kushamiri bila suala hili.
Usipokuwa na moyo wa uvumilivu katika mapenzi basi kila mtu utamuona
hafai. Utamuona hafai na kila siku utakuwa mtu wa kuanzisha mahusiano
mapya. Hayo si maisha sasa!
4. Mahusiano yaliyodumu si kwa kuwa wahusika hawakoseani au makosa
wanayokoseana ni madogo sana. Hapana. Kila binaadamu ana mapungufu yake.
Wote huwa wanakoseana ila tofauti yake na wengine ni kwamba busara na
uvumilivu huwa msingi wa mapenzi yao na ndiyo maana tunaona wanadumu
mpaka leo.
5. Ni binaadamu gani unaweza kuishi naye na msikosane? Ni nani mwenye
uwezo wa kukupa unachotaka kila siku? Hakuna binaadamu wa aina hiyo.
6. Hivyo unavyotaka kuachana na uliye naye suala la kujiuliza ni kuwa
mara ngapi umemueleza kuhusiana na suala unalotaka kumuachia. Na hiyo
isitoshte tu pia jiulize ni sababu gani inayomfanya kutenda suala hilo.
Ukimaliza hapo rudi nyuma na jiulize tena huwa unatumia maneno ya aina
gani katika kumkanya.
7. Maana wengine baada ya kukosewa wao huwa hawawakanyi vyema wenzao wao
bali huripuka kwa maneno makali na dharau. Matokeo yake sasa wahusika
badala ya kuwasikiliza na kufanyia kazi maneno wanayoambiwa kutokana na
makosa yao. wao huwapuuzia na kwaona ni wasema hovyo.
8. Ndiyo, kukosewa kunaumiza sana ila jiulize ni kitu gani kimetokea
bila sababu? Kwenye makosa ya mpenzi wako kuna sababu nyuma yake, hebu
itafute badala ya kulalamika.
9. Mapenzi yasiyo kuwa na uvumilivu ndani yake hayana maisha marefu. Kwa sababu binaadamu ni kiumbe mwenye kukosea.
10 Badala ya kukimbilia kuachana ebu geuka kuwa mwalimu wa mpenzi wako angalau kwa mara chache.
11. Mpenzi wako ni furaha yako kwa maana ndiyo mtu uliyeridhia naye kuwa
naye katika masuala nyeti yahusuyo maisha yako. Sasa kwanini uwe tayari
kumpoteza kisa kachelewa kurudi.
12. Kuwa mvumilivu . Watu wenye hekima ni wavumilivu. Watu wenye kujielewa ni wavumilivu.
13. Ukiwa hauna uvumuilivu kila siku utatangaza ndoa. Leo utaachana na
Mugambara kwa sababu anaongea sana na wasichana ila, jua huyo unaeenda
kuwa naye anapenda sana kitu ambacho hukipendi. Anakunywa pombe je,
utawezana naye? Jibu unalo.
14. Kwa kuwa huyo uliye naye unampenda kwa dhati basi amua kwenda naye
taratibu ukijitahidi kumbadilisha tabia zake. Usiogope, inawezekana,
suala ni uvumilivu na kujiamini tu. Kukubali kumpoteza unayempenda kwa
kukosa uvumilivu ni kujitakia kuingia katika maisha ya kutanga tanga tu.
15. Kumbuka, siku zote wanaovumilia ndiyo huwa wanabaki na ushindi.Bila
uvumilivu Mandela asingekuja kuwa raisi wa afrika kusini.Uvumilivu ni
kila kitu katika maisha.
COMMENT AND SHARE...........................!!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!