AUNTY Ezekiel : Siwezi tena 'ku-kiss' Kwenye Movie
on
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Star wa Bongo Movie nchini mwanadada Aunty Ezekiel, amerudi upya kwenye
tasnia hiyo huku akiweka wazi baadhi ya mabadiliko aliyoyafanya katika
maisha yake kuwa ni pamoja na kutoweza tena 'ku-kiss' kwenye movie
atakazocheza.
Aunty ambaye kwa sasa amerejea na movie mpya inayokwenda kwa jina la
Chritmass Eve, amesema kilichomfanya afikie maamuzi hayo ni majukumu
aliyonayo kwa sasa ya kifamilia ikiwa ni pamoja na malezi ya mtoto.
Akiwa kwenye kipindi cha FNL cha EATV Aunty amesema kuanzia sasa akiwa
kwenye movie, kabla hajakubali ku-kiss na mtu kwanza anamkumbuka mtoto
wake huku akitaja mabadiliko mengine kuwa ni kuweza kuigiza kama 'house
girl' uhusika ambao awali aliwahi kusema hawezi kuuigiza.
"Nimechenji baada ya kuzaa, nimekuwa na mawazo tofauti, nimerudi nyuma
mara mbili hata ikitokea kwenye movie natakiwa ku-kiss, najifikiria sana
hivi mwanangu akiona atafikiria nini" Alisema
Amesema hivi sasa amebadilika kwa kuwa amekuwa mtu mzima na kusisitiza
kuwa kwa sasa ameacha mabo yote ya kitoto aliyokuwa akiyafanya ikiwemo
kuishi kwa skendo maana ameona hayana faida.
Katika hatua nyingine Aunt alisema anatarajia kupata mtoto wa pili ambaye angependa awe wa kike
COMMENT AND SHARE............!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!