
Mrembo aliyekuwa kimya kwa muda mrefu katika uga wa Bongo Movie
mwanadada Aunty Ezekiel amerudi kwa kishindo na kazi mpya ambayo
imemfanya aziponde kazi zake za zamani kutokana na ubora wake.
Aunty aliyekuwa kwenye kipindi cha FNL cha EATV amesema movie ambayo
amekuja nayo sasa ni ya viwango vya hali ya juu, na ina utofauti na
movie zote alizowahi kucheza siku za nyuma kwa kuachana na mambo ambayo
anadai kuwa hayakuwa na maana kwenye movie.
Movie hiyo inayokwenda kwa jina la 'Christmas Eve' ambamo Aunty anatumia
jina la Salome, inazinduliwa leo na itakuwa LIVE kupitia EATV kuanzia
saa 3:00 usiku, ambapo Aunty pia ameeleza sababu za kuifanyia uzinduzi
movie hiyo kuwa ni pamoja na kuwaonesha mashabiki wake utofauti wa movie
hiyo na kazi zake zamani
"Tumefanya kitu tofauti, siyo kama ile ya zamani ya kwenye makochi,
unaingia shikamoo baba, halafu mambo yanakuwa yaleyale, tumeona tuzindue
kwa kishindo ili kuwaonesha watu utofauti" Amesema Aunty.
Katika hatua nyingine Aunty alikiri kuwa yeye ni mjamzito na kwamba
hicho ni kitu ambacho hawezi kuficha wala hana sababu ya kufanya hivyo
kwa kuwa ujauzito haufichiki na pia kuweka wazi kuwa sasa amebadili
mtindo wake wa maisha na kuachana na mambo aliyoyaita kuwa ni ya kitoto.
COMMENT AND SHARE................................!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!