Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe
ametoa salamu za rambirambi kwa Wahanga wa shambulio lililofanywa na
nchi yake katika Bandari ya Pearl, nchini Marekani, miaka sabini na tano
iliyopita.
Akizungumza katika hafla iliyoandaliwa kwenye kituo
cha jeshi la majini la Marekani akiwa sambamba na mwenyeji wake Rais
Barak Obama, Bwana Abe amekiri kukosa la kusema kutokana na uzito wa
ziara yake katika kumbukumbu ya wale wote waliopoteza maisha kutokana na
shambulio hilo.
Ameishukuru Marekani kwa uvumilivu wake na kuongeza kuwa kitisho cha vita hakitajirudia kamwe.
Naye
Rais Obama kwa upande wake ameitaja ziara hiyo ya Waziri mkuu wa Japan
kuwa ni ya kihistoria na kusema kuwa inakumbusha kuwa hata maumivu
makubwa yaliyotokana na vita yanaweza kuleta urafiki na amani ya kudumu.
Amesema baada ya vita mahusiano yao yamekuwa ya amani na nchi zilizokuwa katika ukanda wa Asia Pacifik.
Miezi
saba iliyopita viongozi hao wawili walitembelea pia mji wa Japan,
Hiroshima, ambako Marekani uliushambulia kwa mabomu ya nyuklia.
COMENT AND SHARE......!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!