Madam Wema Sepetu amewatumia ujumbe wa tahadhari wabaya wake wanaomfuatilia anga zake.
Ni ukweli usiopingika kuwa Wema amekuwa akihangaika mara nyingi huku
na kule ili apate mtoto lakini mambo bado yamekuwa yakienda kombo kwa
kuishia kuumia huku baadhi ya watu wakimkejeli kwa matusi wakisahau
jambo la kupata mtoto ni neema ya Mungu pekee.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Wema Sepetu ameweka picha ya Blac
Chyna mwenye ujauzito inayomuonyesha sehemu yake ya tumbo na kuandika,
“Na ningeomba mfunge kweli account zenu ikifika hii hali….
Mxxxxxxiiiuee.”
Mapema mwaka huu ilidaiwa kuwa Wema ana ujauzito wa Idris Sultan
lakini baada ya muda walitoa taarifa za kutoka kwa ujauzito huo japo
haijajulikana kama ilikuwa ni kweli au ni kiki. Usikate tamaa madam Wema
ipo siku machozi yako yatageuka furaha.
COMMENT AND SHARE...........................................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!