Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni
kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume
unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu
mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama
utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi.
Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali
kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha
kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa
muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia
vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na
kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia
"booster". Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako.
Sababu za kukosa nguvu za kiume
Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako
una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada,
unachotakiwa kuzingatia ni chakula bora tu. Wahenga walisema,
utakuwa bora kama chakula unachokula. Je wewe unakula chakula bora ili kulinda heshima yako nyumbani?
Vitu vinavyoweza kupelekea kupungua kwa nguvu za kiume ni kama:
- Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume.
- Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni ya Testosterone
- Kupungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini
Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume
Leo napenda tuangalie vyakula ambavyo vinasaidia kuboresha nguvu za
kiume na kusaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha mapenzi na kulinda
mahusiano na ndoa.
1. Blueberry
Blueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi
hupendelea kuyaita ‘viagra’ asilia kutokana na kazi inayoifanya
mwilini. Blueberries ina virutubishi vinavyoimarisha mishipa ya damu na
kusaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini. Damu ndio kila kitu katika
nguvu za kiume. Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi (
fiber)
ambazo husaidia kuondoa kolesteroli (Cholestrol) mwilini kabla
hazijanganda kwenye mishipa ya damu. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu
husaidia mwanaume aweze kuhimiri mapenzi wa muda mrefu zaidi.
2. Mtini (Figs)
Mtini (figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo
ni kiungo kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ndio
kishawishi cha nguvu za kiume mwilini. Kukosa amino asidi huweza
kusababisha kukosa hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.
3. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters)
Chaza wana kiwango kikubwa cha madini ya zinc. Madini za zinc hutumika katika utengenezaji wa homoni ya
testosterone, shahawa na mbegu za kiume.
Uwingi wa uzalishwaji wa testosterone mwilini huathiri pia hamu ya
mapenzi na nguvu za kiume – ikiwa kidogo huondoa hamu, ikiwa nyingi
hupelekea hamu na nguvu zaidi.
Kupungukiwa kwa madini ya zinc husababisha kupungua kwa nguvu za
kiume, udhaifu (uhanithi), na kushuka kwa kiwango cha uwezo wa kufanya
mapenzi.
4. Karanga
Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa
na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo
wa damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.
5. Vitunguu saumu
Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa
damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye
uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.
6. Ndizi
Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo
kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na
nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo
cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi (
libido).
7. Chocolate
Chocolate inasaidia kuongeza stamina kwenye kufanya mapenzi kwasababu ina viambato vya
phenylethylamine na
alkaloid.
Phenylethylamine ni kiambato kinachopelekea kujisikia vizuri, hasa
wakati wa kufanya mapenzi na alkaloid huongeza stamina na nguvu wakati
wa mapenzi.
Vyakula ni bora kuliko madawa makali
Mie binafsi nashauri kutumia njia asilia katika kutatua matatizo yako
yote ya kiafya. Mwili una njia zake za kurekebisha kila kitu. Ukiona
kuna tatizo inaashiria kuna upungufu ambao unatakiwa kurekebishwa.
Kutumia madawa makali hudhoofisha mwili na hivyo kuupunguzia uwezo wa
kufanya kazi kama inavyotakiwa. Ni vizuri kama utamuona daktari kama
ukiona hakuna kinachowezekana kabla hujaanza kutumia madawa.
Mara nyingi njia asilia hutumia muda mrefu sana kuleta mabadiliko,
lakini matokeo yake hudumu zaidi kuliko kutumia madawa makali ambayo
hutibua mfumo wa kawaida wa ufanyaji kazi wa mwili wako. Mie nashauri
uangalie jinsi unavyokula, nenda kapime vizuri. Kama jogoo ameshindwa
kupanda mtungi,
ruksa kuangalia njia mbadala.
Ni vizuri kula kwa kiasi kabla ya kufanya mapenzi, hasa wakati wa
usiku kabla ya kwenda kulala. Kuvimbiwa husababisha mwili kufanya kazi
ya ziada ya kumeng’enya chakula hivyo kuingiwa na uchovu, uvivu na
kunyong’onyea. Hii husabisha kukosa usingizi na kupungua kwa umahiri
wako katika kufanya shughuli nyingi zinazohitaji nguvu, ikiwemo mapenzi,
kwa ufasaha. Usije kumtafuta mchawi wakati wewe ndio unajiroga, kuwa
makini.
Kama ilivyo ada kwenye mambo mengi ya kiafya, hakuna muarobaini. Ni
vizuri ukajaribu kubadilisha chakula unachokula, fanya mazoezi mara kwa
mara ili kupata mwili wenye nguvu. Kama utakuwa na swali, weka maoni
hapo chini nasi tutakujibu bila kusika hukusu njia zaidi za kutatua
tatizo la nguvu za kiume.
COMMENT AND SHARE.................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!