Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment and dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment and dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment., dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment., dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!!

Vyakula 4 vinavyopunguza uhai wako:;

       
Maisha ni matamu na raha ya wanaijua wale wanaofahamu siri za vyakula. Mie nakudokezea siri mojawapo - chakula bora ni muhimu kwa afya na furaha yako. Bila chakula bora, hakuna raha katika maisha yako hapa duniani.
Mie huwa napenda kusisitiza kuwa tunakula ili tuishi, siyo tunaishi ili tule. Tofauti yake ni kubwa sana, maana wale wanaopenda kuishi ili kula hufakamia chochote ili mradi kiwe chakula, tofauti na wale wanaoishi ili kula maana hujali zaidi afya zao kwanza kuliko njaa, utamu au mvuto wa chakula. Tamaa huwa haiwezi kumfanya asahau vitu muhimu kwenye maisha.
Je wewe uko kwenye kundi gani?
Katika mada yetu ya leo tunaangalia vitu ambavyo kwa namna moja au nyingine hukupunguzia uhai wako maishani. Hivi ni vyakula ambavyo vinaweza kukufanya ukapata magonjwa usiyotarajia, mfano saratani (cancer), kisuraki, na magonjwa ya shinikizo la damu au moyo.

1. Soda


Mara nyingi vinywaji visivyo na vilevi vimekuwa havimo kwenye orodha ya vitu visivyo vya afya. Lakini ukweli ni kwamba, vinywaji vingi sana vinavyouzwa si vizuri kwa afya yako. Mfano mzuri ni soda. Soda ina kiwango kikubwa sana cha sukari. Utafiti umeonyesha kuwa madhara ya soda hayatofautiani na madhara ya kuvuta sigara. Kiwango cha sukari na madawa yaliyomo kwenye soda hukufanyaa uzeeke zaidi kwa muda mfupi.

2. Vyakula vya kusindika


Vyakula vingi vya kusindika huweza kukaa muda mrefu kwa kutumia dawa, sukari, mafuta na chumvi kwa kiwango kikubwa sana. Katika hivi viambato vyote, hakuna hata kimoja kinachokusaidia mwilini bali ni kukuleta madhara zaidi. Hivyo, ili kuwa na afya, punguza kula vyakula vya kusindika, na pendelea kula vyakula asilia, hasa mboga za majani.

3. Nyama (Red meat)       Tokeo la picha la RED MEAT


Kwa muda mrefu sana nyama imegundulika kuwa chanzo cha magonjwa sugu kama magonjwa ya moyo na saratani. Nyama pia siyo nzuri kwa afya sababu husababisha kuongezeka kwa uzito kupita kiasi kama ikiliwa kwa kiwango kikubwa sana.

4. Pombe

Pombe haiitaji maelezo mengi. Kila mtu anafahamu madhara yake ya muda mfupi, ambayo huleta matokeo mabaya zaidi kwa wale watumiaji wa muda mrefu. Pombe, inayonywewa kwa kiwango kikubwa kila mara, hupunguza sana urefu wa maisha sababu huharibu chembechembe muhimu mwilini hivyo kuufanya mwili kukosa kinga, na kudhoofika. Ikifika kiwango hiki inakuwa rahisi kupata magonjwa, na kutoweza kuwa na kinga ya kutosha kuhimili.

Je unawezaje kulinda afya?


Ni vizuri kujali afya, maana kula bila kujali afya ni kama vile unatembea barabarani kwa kufumba macho ukitegemea hakuna baya litakalokutokea. Hivyo basi, ni vizuri ukizingatia haya machache:
  • Pendelea vyakula asilia – hasa mboga za majani na nafaka bora
  • Tumia matunda zaidi, ni bora kuliko juisi au soda za kununua
  • Pendelea kula chakula nyumbani kilichoandaliwa vizuri kwa afya
  • Usitumie kilevi, kama huwezi, basi kunywa kiasi, ili usije haribu afya yako
  • Pendelea kuangalia kiwango cha virutubisho kwenye kila chakula unachokula
  • Hakikisha unakunywa maji kwa kiwango kinachotakiwa
Muone daktari mara kwa mara, ili uweze kupata ushauri wa kitaalamu na matibabu muafaka, kabla tatizo halijawa sugu




COMMENT AND SHARE....................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!

Comments

Facebook Twitter Youtube