WANACHAPWA bakora, wakiwa wamelala ndani wanajikuta wapo nje bila kujua
wametokaje. Hawa ni watumishi wa umma katika Mkoa wa Simiyu, anaandika
Dany Tibason.
Hatua hiyo imeonekana kumkera Jumanne Sagini, Katibu Tawala wa Mkoa wa
Simiyu ambapo amesema, kitendo cha wakazi hao kuwachapa watumishi hao na
na kuwalaza nje kwa njia za kishirikina, kimesababisha wengi wahame
mkoa huo.
Sagini ametoa kauli hiyo mjini hapa jana katika Ukumbi wa Bunge wa Pius
Msekwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa
(LAAC), alipopewa nafasi ya kueleza hali halisi ya mkoa huo kabla ya
kamati kufanya mahojiano na Halmashauri ya Wilaya ya Itilima.
Amesema, wakazi wa mkoa huo wamekuwa na tabia ya kuwachapa watumishi wa
umma wakiwemo walimu hadharani mara wanapokiuka mila na desturi za eneo
jambo ambalo ni kinyeme cha kanuni na sheria za utumishi wa umma.
Sagini ambaye, aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais TAMISEMI,
alifafanua kuwa mbali na watumishi kuchapwa pia wamekuwa wakijikuta
wamelala nje wakati wao walikuwa wamelala ndani.
“Mimi nilipofika pale nimekuta mambo hayo ambayo ni ya ajabu sana,
nimewambia kamwe watumishi hawawezi kukaa na kufanya kazi huku mtabaki
nyuma wakati wote.
“…, kama walimu wanawafundishia watoto wenu wanakuwa madaktari na vyeo
mbalimbali serikali leo mnawachapa fimbo hadharani, nikawambia lazima
mbadilike,”amesema.
Amesema, hali hiyo imesababisha mkoa na halmasauri zake za wilaya kukosa
watumishi ambao ni wataalam na hivyo kuwa katika hali mbaya kiutendaji.
Katibu tawala huyo amesema, wamefika pale lakini hakuna wataalam wa
kutosha na wachache waliopo ni wageni na kwamba, wakipelekwa watalam
wanakaa mwezi, miezi mwaka mmoja na baadaye wanaondoka kutokana na tabia
za wakazi wa eneo hilo.
Amesema, kukosekana kwa wataalam, kumesababisha washindwe kuandaa vitabu
vya LAAC, kushindwa kujibu hoja za Mkaguzi na Mhibiti Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG), hivyo vitabu vilivyokuja mbele ya kamati yako ni vya
hovyo kabisa wala havifai.
Hata hivyo, kamati hiyo ilishindwa kufanya mahojiano na halmashauri
hiyo, kwa madai kuwa imejaa madudu, ubadhirifu hivyo kamati haiko tayari
kuwahoji na kuishia kutoa maagizo.
Sagini aliomba nafasi ili atumie uzoefu alionao kwa kufanya kazi muda
mrefu TAMISEMI, kushirikiana na watendaji waliopo ili waweze kuandaa
upya vitabu vya LAAC, kujibu hoja za CAG na kuziwasilisha kwa CAG kwa
ukaguzi na ndipo warejee tena kwenye kamati hiyo kwa mahojiano.
“Mheshimiwa mwenyekiti, nimeona nizungumze hali halisi iliyopo kwa
utangulizi ili kamati yako ijue ni wapi pa kuanzia na kuishia, binafsi
nimepitia vitabu hivyo sijaridhika kabisa, licha ya kuwa watendaji
wanaweza kuwa wanajiamini na kuwa tayari kuhojiwa ila mimi nasema hakuna
kitu hapa,”amesisitiza.
Kwa upande wake Daudi Nyalamu, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo amekiri
kuwepo kwa vitendo hivyo katika eneo hilo ambapo ameahidi kukaa na
wenzake na kubadili tabia hiyo na kuikomesha kabisa.
“Ni kweli kabisa kama alivyosema, RAS hali halisi ndivyo ilivyo,
watendaji hawakai wanahama mara kwa mara hivyo utendaji kuwa mgumu, haya
ambayo kamati mmetuagiza, tutakwenda kushirikiana na kuyafanyaia kazi,”
amesema.
COMMENT AND SHARE..........................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!