Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
(NACTE) linatoa tahadhari kwa Wamiliki na Wakuu wote wa Vyuo vya Elimu
ya Ufundi nchini kuwa kumeibuka matapeli wanaowaomba fedha au rushwa wakuu wa vyuo
hasa vilivyopewa notisi na Baraza ya kushushwa hadhi au kufungiwa ili
kuweza kuwasaidia kutatua matatizo yao kupitia namba mbalimbali za simu
wanazozitoa.
Baraza linaendelea na kuwatahadharisha
wateja wetu kuwa msikubali kupokea simu zenye kuwaomba fedha au kutoa
kitu chochote wakati mnapotekeleza maelekezo ya Baraza au hata baada ya
kutekeleza maelekezo hayo.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza anatoa
tahadhari hii baada ya ofisi yake kupokea malalamiko hivi karibuni
kutoka kwa baadhi ya Wakuu wa Vyuo na Wamiliki ambao wamedai kupigiwa
simu na watu wanaojitambulisha kuwa Maafisa wa NACTE na kuwadai kiasi
cha fedha kama masharti ya kutatuliwa matatizo yao. Pia Baraza limepokea
taarifa kutoka kwa Wadau wanaolalamika kuwa kuna kundi la watu wanaodai
kupewa fedha ili wasaidiwe kupangiwa vyuo fulani vya ufundi kwa masomo
mbali mbali.
Baraza halina utaratibu wa kuomba
fedha au zawadi ya aina yeyote kwa Mkuu wa Chuo au Mtu yoyote kama
sharti la kupata huduma/msaada fulani.
Ni imani yetu kwamba wakati Baraza
likiendelea na uchunguzi wa kuwabaini matapeli hao ili kuwachukulia
hatua za kisheria, Wadau wetu wataongeza umakini na kuchukua tahadhari
binafsi na watu wa namna hiyo.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji – NACTE
01 Septemba, 2016.
.......................................................................................................................................
COMMENT................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!