Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi za cheti na
diploma na Umma kwa ujumla kuwa lilifunga dirisha la maombi mnamo tarehe
13 Agosti 2016 ili kuruhusu uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa
kozi hizo. Uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa cheti na diploma
ulitarajiwa kutangazwa tarehe 31 Agosti 2016 lakini kwa sababu zilizo
nje wa uwezo wetu umesogezwa mbele mpaka tarehe 5 Septemba 2016.
Baraza pia linapenda kutoa taarifa
kuwa Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) kwa waombaji wa cheti na diploma
utafunguliwa tena tarehe 5 Septemba 2016 hadi tarehe 15 Septemba 2016
ili kujaza nafasi za udahili zitakazokuwa wazi baada ya uchaguzi wa
awamu ya pili. Hatua hii itawezesha kuruhusu machaguo mapya kwa wale
ambao hawakuchaguliwa katika kozi walizoomba pamoja na kuruhusu
waombaji wapya ambao kwa njia moja au nyingine hawakuomba udahili hapo
awali.
Baraza linaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kutokana na mabadiliko hayo.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 02 September, 2016
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!