TAARIFA KWA UMMA
Tunapenda
kuutangazia Umma kuwa tulifunga mfumo wa pamoja wa udahili tarehe 31/08/2016
saa sita usiku ili kuchakata maombi ya waombaji waliofanikiwa kuomba udahili
kwa mwaka wa masomo 2016/2017.
Hata
hivyo kutokana na wengine kushindwa kufanikiwa kutokana na sababu mbali mbali,
Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa awamu ya pili kuanzia tarehe 12 hadi
23 Septemba 2016 ili kuruhusu makundi yafuatayo kuomba udahili.
•
Waombaji
watakaokuwa wamekosa nafasi kwenye awamu ya kwanza
•
Waombaji
wa kidato cha Sita walioshindwa kuomba katika awamu ya kwanza
•
Waombaji wenye vigezo vya Stashahada ambao
walishindwa kuomba kutokana na matokeo yao kuchelewa kufika NACTE kwa wakati,
•
Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya
“Cambridge” mwaka 2016 na matokeo yao yameshatoka,
•
Waombaji
waliofaulu mitihani ya RPL,
•
Waliokuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watakao
kuwa na uthibitisho toka vyuo vyao vya awali.
Baada ya hapo Tume haitaruhusu tena maombi ili kuruhusu
taratibu zingine za kiudahili kuendelea kwa ngazi ya Bodi ya Mikopo na vyuoni.
Asanteni
COMMENT AND SHARE........................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!