Mashabiki wanamtetea mwanamuziki
Chris Brown ambaye anakabiliwa na shtaka la kushambulia baada ya
kumtishia kwa bunduki mwanamke mmoja katika nyumba yake.
Wakili wake anadai kwamba madai hayo ni ya uongo na mashabiki wamekongomana katika mitandao ya kijamii kumuunga mkono.
Hii sio mara ya kwanza kwa Brown kukabiliwa na sheria ikiwemo visa kadhaa vya ghasia alivyotekeleza hapo awali.
Lakini ni kwa nini mashabiki wengi wanampenda?
Chris Brown alimshambulia aliyekuwa mpenziwe Rihanna mwaka 2009 ambapo ilikuwa habari kuu ya mwaka.
Maelezo
ya shambulio hilo katika ripoti ya polisi pamoja na picha za majeraha
ya Rihanna zilifichuliwa katika vyombo vya habari na kusababisha hisia
kali.
Polisi waliitwa makazi ya Chris Brown na mwanamke aliyeomba msaada saa tisa usiku wa kuamkia leo.
Malkia wa urembo, Baylee Curran ameambia gazeti la LA Times, kwamba mwanamuziki huyo alimwelekezea mtutu wa bunduki.
Hata
hivyo walizuiwa kuingia na ilibidi wasubiri hadi kupata idhini ya jaji
kabla kufanya msako wa kutafuta bunduki katika makaazi hayo.
Mwanamke huyo aliyewaita polisi baadaye aliambia vyombo vya habari kwamba walitofautiana na Brown kuhusu majohari.
Alisema
alikuwa ameingia kwa Bw Brown akiwa na rafiki yake na mshirika wa
kibiashara na alikuwa akiangalia mkufu wa thamani uliokuwa umevaliwa na
mwanamume mmoja pale mwanamuziki huyo alipomkaripia na kumtaka aondoke
mara moja akiwa amemwelekezea bunduki.
COMMENT AND SHARE.....................................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!