Mimi ni mpenzi mkubwa wa muziki na hasa muziki wa dansi ingawa nyimbo
nyingi sizijui. Nikiwa mdogo nilikuwa napenda sana kuwasikiliza
Washirika Tanzania stars na mpaka sasa nikisikia nyimbo yao yoyote
natulia kwa makini kusikiliza. Hiyo ilikuwa bendi pendwa kwangu kabla
hawajasambaratika na kujikuta nikitekwa na wakongo hasa hasa Wenge
Musica BCBG na kidogo ikaingia Nouvelle Generation.
Waliposambaratika hao nilijikuta katika majonzi baadae nikapata faraja
kwenye nyimbo za dini. Bado nafuatilia muziki ila si kwa nguvu ile tena,
itokee tu (in sheikh Kipozeo tone).
Niingie kwenye mada. Muziki wa Tanzania umekuwa kwa kiasi kikubwa na
unapozungumzia mastaa wanaotamba vilivyo utawakuta Ali Kiba na Nasib
Abdul a.k.a Diamond Platnumz. Watu hawa wamejijengea umaarufu mkubwa na
kujitengenezea mashabiki ambao wamegeuka mahasimu wakubwa kwenye
mitandao ya kijamii hasa instagram.
Mimi binafsi si shabiki wa mtu yoyote kati ya hao ila kuja mmoja akitoa
wimbo wake (hit song) najikutaga nafuatilia mwenendo wake kwa mashabiki
na vyombo vya habari. Kimsingi Alikiba alivuma sana kabla ya Diamond na
alifanikiwa kufanya show nyingi nje ya nchi hususan Uingereza na
Marekani ambapo nahisi ilikuwa mwanzo wake wa kuporomoka kimziki kabla
hajaamshwa na watu wanaomchukia Diamond na kumtengeneza kama mtu
atakayemshusha Diamond kimuziki.
Alikiba amesahau kazi yake kama mwanamziki amejikuta kwenye harakati za
kupambana kumshusha mwenzake ili akae kileleni. Hii itaugharimu muziki
wa Tizii kwani kushuka kwa Diamond hakutamuweka Ali Kiba juu kivile kwa
kuwa hajui kukaa kileleni. Katika harakati zake za kumshusha Diamond
kileleni amejikuta yeye na timu yake wakijaribu ku counter pale Diamond
anapoachia hit song mpya.
Kitu kilichonisukuma kuandika huu uzi ni baada ya Diamond kuachia wimbo
wake wa Salome ambao ni remix ya wimbo Maria Salome wa Saida Karoli.
Siku moja baada ya kuachia wimbo huo Alikiba naye akaachia wimbo wake wa
Nitulize. Nimezisikiliza nyimbo zote mbili kwa kiasi ila nimefuatilia
ni kwa kiasi gani nyimbo hizo zimepokelewa na mashabiki na kugundua
Alikiba amefanya Tuming mbaya sana.
Ni afadhali angeacha Salome akakaa hewani kwa wiki moja au mbili ili
atoe yake. Sio uongo kuwa Diamond ana mashabiki wengi across the
continent na hayo yanathibitishwa na kauli ya wanamuziki wenzake wa
Afrika kama akina Mafikizolo na Davido. Labda niongee kidogo, Jumatatu
nilikuwa niko bored nyumbani na wife hayupo kaenda msibani nikawa
naangalia chanel hazinivutii baadae nikajikuta nimeweka chanel E.
Hapo nilikuta Mafikizolo wakiwa wanahojiwa walivyomtafuta Davido. Baada
ya kumpata Davido ili wafanye collabo aliwaambia pia wamtafute Diamond
kwani ni mtu mwenye mvuto kimuziki na ana mashabiki wengi ambapo kila
msanii wa Afrika anatamani kuwa kama Diamond. Hiyo testimony inanipa
fursa ya kusema Diamond yuko mbali sana kimuziki kuliko Alikiba.
Mwisho nakuomba msomaji uangalie youtube mapokezi ya Salome na Nitulize
halafu uniambie nani anafanya vizuri. Alikiba alipofanya vizuri alirudi
kulala na kushtuka underground wake kawa leader wake. Akitaka kufanikiwa
ajiwekee malengo ya kutoka alipo kusogea mbele na si kumkimbiza mtu.
Na pili akumbuke yeye yuko chini ya lebo ya watu wengine ( sony) wakati
mwenzake anafanya muziki chini ya lebo yake mwenyewe kwa hiyo sijui kama
hiyo itamtengenezea wigo wa kuwa na lebo yake kama anavyojaribu kufanya
kwa kuwachukua baadhi ya wanamuziki kama Baraka da Prince kuwa ndani
yake.
COMMENT AND SHARE.............................!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!