
Wakati viongozi wa dini wakiendelea na jitihanda za kusaka suluhu kati
ya upande wa Serikali na Chadema kuhusu namna ya kuzuia kwa amani
kufanyika kwa Operesheni ya chama hicho iliyopewa jina la UKUTA,
Septemba 1, Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ametoa
maoni yake.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema kuwa haoni haja ya
kufanyika kwa vikao hivyo vya kusaka maridhiano kwani Chadema
wanachotaka kufanya kiko kikatiba.
“Sioni ni kwanini tunahangaika na vikao vya maridhiano na tahariri
nyingi kuhusu shughuli ya CHADEMA kufanya operesheni yao ya UKUTA.
Kuandamana ni Haki ya KIKATIBA. Tuache watu watimize Haki yao Kwa amani.
Kuzuia watu kufanya jambo lao la kikatiba ndio kuvunja amani. Wanaotaka
kuandamana waandamane na wanaotaka kufanya Kazi zao nyingine tuendelee
na Kazi zetu. Kwanini kutekeleza Haki ya kikatiba iwe ni kuvunja amani?
Kwanini?,” Zitto ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Hata hivyo, vikao vya maridhiano vinavyoendelea tayari vimeonesha kuzaa
matunda kwenye suala la mgogoro wa Bunge ambapo wabunge wa vyama vya
upinzani wameridhia kurejea Bungeni katika vikao vitakavyoanza mapema
mwezi ujao.
Serikali imeendelea kuwaonya watu wote wanaopanga kuandamana Septemba 1
huku viongozi wa Chadema wakisisitiza kuwa siku hiyo watafanya
maandamano kama walivyopanga.
Hali hiyo imepelekea kumtoa hadharani Kingunge Ngombale Mwiru ambaye
ameomba marais wastaafu kumshauri Rais Magufuli ili kuruhusu Serikali
kukaa na Chadema kusaka muafaka wa masuala ya kisiasa nchini.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!