Kumekuwepo na wimbi kubwa kwa hawa dada zetu, kuwa na watoto bila
mume.Ukimuuliza anakwambia tumeachana na hawakotayari kuweka wazi sana.
Sasa mimi nashindwa kuelewa tatizo ni sisi wanaume, au ni hawa dada zetu?
Na je mwanaume inakuweje mpaka unafikia hatua ya kumwachia watoto mzazi mwenzio?
Na wewe dada inakuweje uone unaweza muishi na watoto bila mume hata kama hela ya kuwalea unayo?
Yaani jaribuni kuchunguza katika wasichana kumi hapa Bongo, wenye
umri 25-35 saba wana watoto na ukiuliza kuhusu baba wa mtoto, au watoto
utapewa ngonjera tu!
Tatizo liko wapi? Ebu fungukeni kina dada au sababu ni sisi wanaume?
COMMENT AND SHARE........................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!