Kamishna wa mawasiliano nchini Uingereza anachunguza uamuzi wa programu ya WhatsApp wa kugawana data na kampuni ya facebook.
Data hiyo ya watumiaji wa WhatsApp itatumiwa kuvutia matangazo yanayoonekana na watumiaji wa mtandao wa facebook.
Itagawana nambari za simu na maelezo ya mara ya mwisho mteja kuingia katika akaunti yake ya WhatsApp na facebook.
Kamishna
huyo amesema kuwa kwa kuwa mabadiliko hayo yataathiri watu wengi
,anataka maelezo zaidi kuhusu kile kitakachogawanywa kati ya huduma hizo
mbili.
Kamishna Elizabeth Denham amesema kuwa watumiaji watakuwa na maoni tofauti kuhusu mabadiliko hayo.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!