Wema Sepetu Ampigia Magoti Idriss Sultan:;

Uhusiano wa Wema Sepetu na Idris Sultan unaanza kutukumbusha ule wa
Chris Brown na Karrueche Tran ule wazungu wanauiita ‘off and on.’
Baada ya hivi karibuni kuzinguana tena hadi kumfanya Idris ajiondoe
Instagram hadi sasa, wawili hao wanaonesha kuanza kutafuta suluhu.
Wema amepost picha hiyo juu Instagram inayoonesha walikuwa wakiwasiliana kutumia app ya Facetime, aliandika:
That moment you realise how much u miss a special someone… Rudi basi… hata kidogo tu… 😔
Wawili hao waliingia kwenye mgogoro baada ya Wema kuisusia show ya
Idris, Funny Fellas kwa mara nyingine tena huku mshindi huyo wa Big
Brother akihudhuria za mpenziwe, ikiwemo Black and Tie iliyofanyika
mwezi uliopita.
Baada ya kuchoshwa na tabia ya mpenzi wake kutompa support kwenye show
zake, Idris naye aliamua kuipotezea show ya Usiku wa Vigoma
iliyoandaliwa na Sepetunga mwishoni mwa wiki – na hapo ndipo mambo
yalipoharibika.
Mashabiki wa Wema walikasirika baada ya shemeji yao kuikwepa show hiyo
na wanamshambulia Instagram. Kutokana na kuandamwa, Idris amelazimika
kuongea:
Sipendi kuona watu wakiingia na kuongea kama wanajua maisha yangu na
watu wangu wa karibu, makosa wakifanya wengine mnakuja kwangu mnaanza
“Ndio asingefanya vile kama sio wewe kufanya hivi” mnakazana kusema eti
naposti wanawake mara ooo porojo kibao. Sina freedom ya kumpost dada
angu ? Kweli ? Au rafiki yangu kazindua brand mpya siwezi mpost
nikampongeza?
Mnauliza kwanini sijaenda vigoma nimesema because show yangu hakuja
hata moja na nimeenda show zake zote na yeye halalamiki because anajua
nimesema siendi fair enough mbona hamjaongelea hilo? I repeat nikikaa
kimya is for a pure reason that it’s not anyones business this is my
personal life kama mnaongeleaga fair basi mngefanya kuuliza kwanini
mpaka am selling out hajaja.
“Give me a break sina maisha ya kuigiza lets have respect for each
other bana. Na nimesema msiniite shemeji for one big good reason, imekua
too much i am a brand na jina idris linamezwa na shem, ningejua this
from the beginning nisingeruhusu mniite tangu mwanzo so msiwe kila kitu
mnafikiria negative tu. Na sikuwa na haja ya kuandika yote haya pia
TusichukulianePoa.
Hata hivyo Wema naye alimpigilia msumari wa moto Idris kwa kupost picha
ya wanaume anaowapenda #MCM (Man Crush Monday) na mmoja wao ni Diamond.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!