Wema Akanusha Kurudiana na Diamond, Awasifia Zari na Tiffa:;
Wema, Diamond na Zari
Mambo mengi yametokea wiki hii kuanzia Wema Sepetu kuachana na mpenzi
wake Idris Sultan hadi Miss Tanzania huyo wa mwaka 2016 kuhudhuria
birthday party ya binamu wa Diamond, Romeo na kukutana na vijana wa WCB.
Kutokana na Wema kujumuika na vijana wa himaya ya WCB, kumezuka tetesi
kuwa huenda ukaribu kati ya muigizaji huyo na Diamond unaweza ukawa ni
zaidi ya maex wawili walioamua kuacha bifu zao zipite.
“Yaani watu wakianza tu kuongea vizuri, bifu zao zikiisha wamerudiana,
maisha lazima yaendelee, mwisho wa siku hatuwezi kuwa tunakaa
tunachuniana miaka yote tutakayoishi, life is too short,” Wema
alimweleza Soudy Brown kupitia U Heard ya Clouds FM.
“Mimi mwenyewe najisikia hadi amani kwamba there is no beef, maisha
yanaendelea, mimi sijarudiana na Diamond, mimi namrespect kama msanii,
nampenda Diamond kama msanii and I love his music and I am so glad
tumeweka all this behind,” aliongeza.
Kuhusu kama anampenda mtoto wa Diamond, Tiffah, Wema alisema, “Tiffah
amenikosea nini katika maisha yangu? Nimchukie Tiffah si nitakuwa
mwendawazimu jamani,” alisisitiza.
Kuhusu tetesi kuwa aliwahi kumuita Tiffah zombie kama Zari alivyowahi
kudai lakini Wema amezikanusha, “Hayo maneno sio ya kwangu, sijawahi
hata siku moja, kwanza the way I adore babies, siwezi nikamuita baby
zombie hata awe vipi.”
Kuhusu Zari staa huyo alisisitiza kuwa hana bifu naye.
“Mimi sina bifu na Zari na sijawahi kuwa na bifu na mwanamke wake yeyote
Nasib, kwasababu huwa naona matatizo yangu mimi na Nasib ni mimi na
yeye, Zari hana makosa, katongozwa, amedetiwa, amewekwa ndani, hana
makosa hata kidogo huyo mwanamke.”
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!