
Unataka kwenda jela? Ni rahisi, weka picha za ngono mtandaoni, na utakuwa mkazi wa huko kwa kipindi cha miaka 20.
Kwa mara nyingine tena, mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA imewakumbusha watanzania kutozichezea sharubu za sheria ya makosa ya mtandaoni, lasivyo wataishia pabaya.
“Ni vyema wananchi wakatambua kwamba uchochezi kwenye mitandao kwa
kusambaza ujumbe wenye viashiria vya uvunjifu wa amani au kuweka picha
zisizofaa kwenye mitandao sheria ipo wazi na watu watajikuta wanaishia
pabaya, hivyo ni vyema kuchukua tahadhari mapema,” alisema Mhandisi wa
Mawasiliano wa Victoria Rulakara wakati akizungumza kwenye kipindi cha
Hotmix cha EATV.
Wakati huo huo, mamlaka hiyo imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu
matumizi sahihi ya mitandao ikiwa ni pamoja na kuwaonya watu wanaonzisha
blog zenye majina ya uongo kutukana watu wengine.
Sheria ya Makosa ya Mtandaoni ilipitishwa mwaka jana na rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete.
COMMENT AND SHARE..................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!