Watu 38 wafariki kutokana na tetemeko la ardhi Italia:;
Watu takriban 38 wamefariki na
wengine 150 hawajulikani walipo baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi
lenye nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Richter katikati mwa Italia,
taarifa zinasema.
Watu wengine wengi wamefukiwa chini ya vifusi.
Wengi
wamefafiki katika kijiji cha Pescara del Tronto ambacho kimeharibiwa
vibaya na inahofiwa kwamba idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka.
Tetemeko
hilo lilitokea mwendo wa saa tisa na dakika thelathini na sita usiku
saa za Italia (01:36 GMT), 76 km (maili 47) kusini mashariki mwa mji wa
Perugia, katika kina cha 10km (maili sita) chini ya ardhi, taasisi ya
Marekani inayohusika na mitetemeko ya ardhi USGS imesema.
Mitetemeko
ilisikika katika miji ya mbali kama vile Roma, Venice, Bologna na
Naples. Mjini Roma, baadhi ya majumba yalitikisika kwa sekunde 20, kwa
mujibu wa gazeti la La Repubblica.
Mji wa Amatrice nao pia uliharibiwa vibaya. Watu wanne wanahofiwa kufariki katika mji jirani wa Accumoli.
Eneo
hilo, ambalo linapatikana katikati mwa mikoa ya Umbria, Lazio na
Marche, ni maarufu sana kwa watalii na kuna wageni wengi waliokuwa eneo
hilo kipindi hiki cha shughuli nyingi za kitalii.
Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa katika mji wa Norcia, karibu na Perugia.
Waziri mkuu wa Italia, Matteo Renzi, amesema serikali yake inaendelea kuwasiliana na taasisi za kiraia la ulinzi wa nchi hiyo.
Meya wa mji wa Amatrice Sergio Perozzi ameambia kituo cha redio cha serikali cha RAI kwamba mji huo umeharibiwa vibaya.
"Barabara
za kuingia na kutoka mjini hazipitiki. Nusu ya mji imeharibiwa. Watu
wamefukiwa chini ya vifusi… kumetokea maporomoko ya ardhi na kuna daraja
moja ambalo huenda likaporomoka," amesema.
Shirika la kulinda raia Italia limeeleza tetemeko hilo kuwa "mbaya"
Tetemeko hilo awali lilikisiwa kuwa la ukubwa wa 6.4. Lilifuatwa na mitetemeko mingine mikubwa, gazeti la
La Repubblica limeripoti.
USGS wamesema uharibifu huenda ukawa mkubwa.
Mwaka
2009, tetemeko la ardhi la nguvu ya 6.3 lilitokea eneo la Aquila, na
kusikika pia katika mji wa Roma. Watu zaidi ya 300 walifariki.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!