Watoto waingizwa kwenye jeshi Sudan Kusini:;
Serikali ya Sudan Kusini imewaajiri watoto wavulana kama wanajeshi
wakati huu inapojiandaa kwa mzozo mpya, kwa mujibu wa shirika la
Associated Press.
Mwanasiasa mmoja mwenye ushawishi anaripotiwa
kuongoza shughuli ya kuwaajiri watoto hao, wengine wakitajwa kuwa na
umri wa hadi miaka 12 kutoka kijiji kimoja nchini humo.
Nyaraka
zinaonyesha kuwa shughuli ya kuwaajiri watoto hao, ilifanyika muda
mfupi baada ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kuidhinisha azimio
wiki moja iliyopita la kutuma wanajeshi 4000 kwenda Sudan Kusini,
kuwalinda raia baada ya kuzuka mapigano mapya katika mji mkuu Juba mwezi
uliopita.
Mapigano hayo yamekuwa kati ya vikosi watiifu kwa rais
Salva Kiir na vile vya makamu wake aliyefutwa kazi Riek Machar ambaye
tayari ameikimbia nchi hiyo.
Shirika la kuwahudumia watoto la umoja wa Mataifa UNICEF linasema
kuwa zaidi ya watoto 650 wameajiriwa na makundi yaliyojihami nchini
Sudan Kusini tangu mwanzo wa mwaka huu.
UNICEF sasa ina hofu kuwa
mzozo huo mpya huenda ukahatarisha maisha ya maelfu ya watoo na kutaka
shughuli hiyo ya kuwajiri watoto isitishwe mara moja.
Pia
inakadiriwa kuwa watoto 16,000 wameingizwa kwa makundi yaliyojihamia na
pia jeshini tangu mzozo nchini Sudan kusini uanze mwezi Disemba mwaka
2013.
Akiongea baada ya kufanya ziara katika maeneo ya Bentiu na
Juba nchini Sudan Kusini, mkurugenzi mkuu wa UNICEF Justin Forsyth,
alisema kuwa kuna hofu kuwa huenda watoto zaidi wakaingizwa jeshini.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!