WAZIRI wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Augustine Mahiga amesema Watanzania wengi wanashikiliwa katika
magereza ya Afrika Kusini kwa makosa ya kujishughulisha na biashara ya
dawa za kulevya.
Alisema hayo wakati akifafanua suala la Watanzania wanaoishi nje ya
nchi, hasa vijana na kusema wamekuwa wakijishughulisha na uuzaji dawa za
kulevya badala ya kuwa raia wema.
Aliwataka kuacha kujishughulisha na mambo yanayoweza kuwaweka kwenye wakati mbaya na kutii sheria za nchi waliko.
Alisema Watanzania wengi waliopo Afrika Kusini wanafanya kazi ya
kusafirisha dawa za kulevya na wengine wanasubiri ‘kuzamia meli’ mjini
Durban.
Alisema suala hilo ni moja ya mambo ambayo yamekuwa yakijadiliwa na
Serikali ya Afrika Kusini ambapo Tanzania imejulishwa tatizo hilo na
Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Afrika Kusini pamoja na Rais Jacob
Zuma.
“Ni kweli lipo tatizo kubwa la Watanzania waliopo Afrika ya Kusini
kujishughulisha na biashara ya dawa za kulevya. Serikali ya Afrika
Kusini imetujulisha jambo hilo nasi tunalishughulikia kuiepusha nchi
kuwa na uhusiano mbaya wa kidiplomasia na nchi nyingine.
HATARI SANA..
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!