Watakao Chakachua Mitihani Kidato cha Nne Kukiona:;
WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako
amesema haafiki uchakachuaji kwenye mitihani na kusema wakuu wa shule
watakaobainika kufanya udanganyifu huo hawatapona.
Profesa Ndalichako alisema hayo kwenye kikao kati ya Ofisi ya Rais,
Tamisemi, Maofisa Elimu wa Mikoa, Wakuu wa shule kongwe na wakuu wa
shule zilizoungua moto.
Alisema ikiwa imebaki miezi mitatu kwa wanafunzi wa kidato cha nne
kufanya mitihani aliwataka wakuu wa shule kujipanga kupata ufaulu mzuri.
“Bado siafiki suala la uchakachuaji kwenye mitihani wanafunzi waachwe
wafanye mitihani wenyewe na si kupitia kamati za ufundi, sasa Wizara
inaangalia ubora wa elimu na wakuu wa shule watakaokiuka agizo hilo
watachukuliwa hatua,” alisema.
Alisema pia matokeo ya mitihani ya shule za sekondari ya mwaka jana
yalimhuzunisha sana lakini anaamini wakuu wa shule watajipanga
kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri zaidi.
“Nilipokuwa Baraza la Mitihani nilisema nisiulizwe kutokana na matokeo
kuwa mabaya lakini sasa niko Wizara ya Elimu siwezi kukwepa hilo tena,”
alisema.
Waziri Ndalichako alisema watabadilisha mfumo wa namna maofisa elimu
watakavyofanya kazi zao ili kuongeza kiwango cha ufaulu katika shule za
serikali na kuwataka wakuu wa shule na maofisa elimu kila mmoja
ajipange.
Aidha alisema mkuu wa shule ni mdhibiti wa taaluma katika eneo lake na
hatakiwi kumuogopa mtu anayemuongoza. Waziri huyo pia alisema katika
mtihani wa kidato cha sita uliopita shule 100 za kwanza shule za
serikali zilikuwa tatu na kuwa nafasi ya 53 ndio ilishikwa na Ilboru ya
Arusha.
“Mpaka namba 100 shule za serikali ni tatu tu, sio kitu cha kawaida hapa
ndio mahali pa kuzungumza kama serikali tunashindwa kuonesha mfano
tuachie sekta binafsi,” alisema
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!