Wataalam hamsini wa masuala ya
usalama ambao kwa pamoja wamewahi kuhudumu katika utawala wa
Republican wameonya kwamba Donald Trump"atakuwa rais asiekua makini
zaidi " kuwahi kuhudumu katika historia ya Marekani.
Katika waraka wao wa wazi wanasema Bwana Trump "hana haiba, maadili wala uzoefu " wa kuongoza nchi.
Kundi
hilo la wataalam wa masuala ya usalama linajumuisha mkurugenzi wa
zamani wa idara ya ujasusi ya Marekani CIA Michael Hayden na wakuu wa
zamani wa usalama wa ndani wa nchi.
Wengi wa waliotia saini waraka huu kuhusu Trump walikataa kusaini waraka kama huo mwezi Machi.
Bw
Trump amejibu kwa kusema kuwa waraka huo ni wa wasomi wa Washington
waliofeli ambao amesema wanapaswa kulaumiwa kwa kufanya dunia kuwa
mahala hatari.
Bw Trump amekiuka sera ya kigeni ya Republican mara kadhaa.
Mgombea wa chama cha Republican amehoji ikiwa Marekani inapaswa
kuheshimu wajibu wake kwa NATO, kuidhinisha mateso na kupendekeza
kwamba Korea Kusini na Japan wanapaswa kujihami kwa silaha za nyuklia .
"Alithoofisha mamlaka ya Marekani inayojitambua kama kiongozi
wa dunia huru ," ulieleza waraka wa wakuu hao wa zamani wa usalama.
"Anaonekana
kukosa uelewa wa kimsingi kuhusu imani katika katiba ya Marekani,
sheria za Marekani na taasisi za Marekani ,ikiwemo uhuru wa kidini,
uhuru wa vyombo vya habari, na uhuru wa mahakama. ."
"Hakuna hata mmoja wetu atakaempigia kura Donald Trump," ilielezea barua.
Katika
kauli yake Bwana Trump amesema majina ya wale walioandika waraka huo
yalikua "ya wale ambao wamarekani wanapasa kuwatafuta kupata majibu ya
kwanini dunia imeharibika".
"Tunawashukuru kwa kujitokeza ili
kila mmoja nchini atambue ni nani anapaswa kulaumiwa kwa kuifanya dunia
kuwa mahala hatari kiasi hiki ," aliendelea.
" Si lolote hao
zaidi ya wasomi walioshindwa kazi ambao wanataka kuendelea kushikilia
mamlaka na ni wakati sasa wa kuwawajibisha kwa vitendo vyao."
Pia
miongoni mwa wale waliotia saini waraka huo ni pamoja na John
Negroponte, mkurugenzi wa kwanza wa idara ya ujasusi na baadae naibu
waziri wa mambo ya nje; Robert Zoellick, ambae pia alikuwa naibu waziri
wa mambo ya kigeni na rais wa zamani wa Benki ya dunia ; na mawaziri wa
zamani wa usalama wa ndani ya nchi , Tom Ridge na Michael Chertoff.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!