Wataalamu Wanasema Hivi:;

s for
Me and My House we
will serve the
Lord
(Joshua 24:15)
Kuna wataalamu 600 wa masuala ya ndoa (marriage experts) walikaa pamoja kujadili misingi (fundamentals) muhimu ya ndoa ambayo wanandoa wakiifuata ndoa zao zitakuwa imara na zenye afya hadi kifo kitakapowatenganisha.Misingi hiyo ili imeinamia zaidi kwenye imani ya
Kikristo, ingawa mtu yeyote bila kufuata dini yake anaweza kuifuata na bila shaka ndoa yake itakuwa ya tofauti.
Kuna
mambo mengi sana muhimu ya kufanya katika ndoa ili ndoa iwe imara na
yenye mafanikio, hawa wataalamu walichambua yale ya mambo msingi tu
ambayo yakifuatwa basi vitu vingine muhimu katika ndoa inakuwa ndani
yake.
Tumeshayaongea sana haya mambo hapa kwenye blog hii inaweza
kuonekana kama kurudia, hata hivyo kuna kitu muhimu na kipya unaweza
kukipata hapa leo.
Je, ni Misingi ipi hiyo?Kwanza - Kristo kuwa Kiongozi wa NdoaNdoa ambayo inaendeleza, ongeza, imarisha na kufurahia mahusiano na Yesu Kristo itakuwa na picha kamili ya Yesu na kanisa.
Kila
mwanandoa atakuwa na uhusiano mzuri na Kristo na atajitahidi kufanana
na Kristo na matokeo yake dhambi itakaa mbali na dhambi kukaa mbali basi
upendo wa kweli wa kimungu huongoza ndoa.
Ndoa yenye msingi wa Kristo huwa na maombi na maombi ni mawasiliano ya wanandoa na Mungu, hivyo kwa kuwa na
connection kati ya Mungu na wanandoa, Mungu atakuwa anaipa
stabilization ndoa yao kila wanapokutana na tatizo, shida au jaribu.
Unajua kuna siku shetani huwa anaamua kupaka matope (mavi)
mmoja ya wanandoa ili asipendwe (unajisikia kutovutiwa na mwenzako), ni
kwa maombi tu unaweza kuharibu kazi za aina hii za shetani si pesa,
wala elimu wala ujanja.
Kwenye ndoa kuna good times na bad times na Kristo huweza kuwapitisha wanandoa vizuri kama wanamtegemea yeye, hilo halina ubishi ni amini na kweli.
Pili - Upendo wa KujitoaMaisha
ya binadamu ni safari ndefu, si sahihi kwamba siku zote ndoa itakuwa na
mapenzi yaleyale ya motomoto, au kupendana kule kule kama mwanzo,
kiwango cha mahaba kupanda tu graph kila iitwapo leo; si kweli, kutokana
na kuwa na malezi tofauti na mambo mengine inawezekana ndoa kupita
kwenye wakati mugumu sana, kuna stress, kuna kukata tamaa, kuna business
kufilisika, na kuwa wakati tu inatokea mume na mke kila mmoja hampendi
mwenzake bila sababu, hivi vyote vinahitaji watu wenye Upendo wa kujitoa
ili kurudi kwenye mstari.
Katika ndoa conflict na disagreement hutokea bila upendo wa kujitoa basi ndoa haiwezi kufika popote.
Kwenye ndoa hakuna mtu perfect wote bado tuna tumia Learner driving license kwa maana kwamba tunaendelea kujifunza na kutoa efforts za kuhakikisha ndoa inakuwa na afya na inaendelea kudumu na kudumu na kudumu.
"A house divided against itself can not stand"
Kuna
utafiti ulifanywa kwa wanandoa waliopata talaka, asilimia 40 walisema
wanatamani kurudi kwenye uhusiano wao wa kwanza, hii ni kuthibitisha
kwamba wangekuwa na upendo wa kujitoa basi wasingeamua kuomba talaka zao
kwani kuna watu ambao conflict kidogo tu, tuachane!
Hawana dogo na wengine sasa kuoa na kuolewa ni kama shopping!
Tatu - MawasilianoUtafiti unaonesha kwamba watoto wadogo wa kike wamebarikiwa sana (talented) na uwezo wa kuongea na lugha kwa ujumla (linguistic), huweza kuongea haraka na mapema kuliko watoto wadogo wa kiume.
Hiyo
tabia huendelea hadi wanapokuwa watu wazima na kwa maana hiyo wanawake
na wanaume lipokuja suala la kuongea na mawasiliano kwa ujumla kuna
tofauti kubwa.
Inajulikana kwamba wanawake huongea maneno kati 40,000
hadi 50,000 kwa siku wakati wenzao wanaume huongea maneno 15,000 hadi
25,000 kwa siku.
Hivyo basi wanawake ni viumbe wanaohitaji mwanaume
kuuongea ili na yeye aongee hayo maneno yake, ndiyo maana kwa mfano kama
umetoka kazini basi mwanamke anapenda sana umwambie mambo mbalimbali
kama vile unafikiri kitu gani, nini kilitokea kazini, watoto
wameshindaje, unajisikiaje kuhusu yeye mwanamke nk.
Wakati huohuo wanaume hujisikia sawa tu hata asipoongea chochote akifika nyumbani kutoka kazini matokeo yake mke anakuwa bored na hayo ni mawasiliano mabovu.
Wanaume kushindwa kuelezea hisia zao kwa wake zao ni kitu kinachowaumiza sana.
“Show me a quiet reserved husband, I will show you a frustrated bored wife”
Panga muda maalumu kwa ajili ya maongezi ya maana na mke wako hata kwa kuwa na matembezi au outing.Hata hivyo wanawake wanapaswa kufahamu kwamba kuna wanaume ambao hawawezi kuwa kama wanavyotaka wao kwani ndivyo walivyo.
Mume
wako hataweza kukutimizia mahitaji yako yote kwani hakuna mwanaume
duniani ambaye anaweza kumpa mwanamke vyote anavyohitaji, ndiyo maana
hata wewe mwanamke mwenyewe hupo perfect mia kwa mia.
Kumbuka
Unapowasiliana na mume au mke;Badilisha kile ambacho kinaweza kubadilishwa
Elezea kile ambacho anaweza kukielewa
Fundisha kila ambacho anaweza kujifunza
Patanisha kile ambacho anaweza kukubaliana
Rudia kile ambacho anaweza kukiimarisha.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!