WASANII
mbalimbali wanaopenda amani wameungana kwa pamoja kupinga maandamano ya
UKUTA yanayotarajiwa kufanyika Septemba Mosi, mwaka huu.
Akizungumza
jana mbele ya Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Wasanii hao wapenda
amani, Steve Nyerere alisema hamna haja ya maandamano bali tunahaja ya
kufanya kazi hususan kwa vijana.
"Vijana
ndio muhimili mkubwa kulinda amani ya nchi,tusiwaze maandamano bali
tuwaze je Akinamama na Watoto wanapata huduma hospitali"alihoji Steve Nyerere.
Kwa
Upande wa Makamu Mwenyekiti wa Wasanii hao, Asha Baraka alisema
wameamua kupaza sauti zao kwa niaba ya Wasanii wote wanaopenda amani.
Alisema Tanzania ni nchi ya Amani sio nchi ya vita hivyo wanapofanya shughuli za UKUTA shughuli zote za kijamii zitasimama.
Hatahivyo
aliomba Septemba 1, UKUTA wasimamishe maandamano hayo, pia watafute
njia muafaka ya kuweza kuongea Vyama kwa Vyama na wakapata muafaka ili
nchi iweze kwenda mbele.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!