Mbwa
kwa jina Duke amechaguliwa kwa mara ya tatu kuwa meya wa mji wa
Cormorant jimbo la Minnesota, tunaangazia wanyama wengine ambao wamewahi
kuchaguliwa kushikilia nyadhifa mbalimbali au kufanya kazi nyingine za
binadamu. Mbwa achaguliwa tena kuwa meya Minnesota, Marekani 1. Mbwa waliowahi kuchaguliwa kuwa mameya Kuna Junior Cochran, mbwa mweusi aina ya Labrador, aliyechaguliwa kuwa meya mji wa Rabbit Hash, Kentucky, mwaka 2004.
Na hatuwezi kumsahau Bosco mbwa aliyehudumu kama meya wa Sunol, California, kuanzia 1981 hadi 1994.Hata kuna sanamu ya ukumbusho wake.
Sanamu ya mbwa aliyejulikana kama Bosco
2, Paka waliochaguliwa kuwa mameya Paka kwa jina Stubbs alichaguliwa meya wa Talkeetna, Alaska, mwaka 1997. Kuna
hata akaunti ya Twitter yenye jina lake. Kwenye maelezo imeandikwa:
"Mimi ni paka. Nilichaguliwa Meya wa Alaska. Karibuni, nitakuwa rais."
Paka kwa jina Stubbs
3. Kifaru 'taka' aliyechaguliwa kuongoza Sao Paulo Mwaka 1959, kifaru wa umri wa miaka mitano kwa jina Cacareco alichaguliwa meya wa mji wa Sao Paulo kwa kura nyingi sana.
Cacareco,
jina ambalo maana yake ni "taka" kwa Kireno, aliandikishwa kwenye kura
kama hatua ya kulalamikia ufisadi miongoni mwa wanasiasa. Hakuchukua mamlaka hata hivyo kwani uchaguzi ulirudiwa. 4. Mbuzi kiongozi wa New Zealand Iwapo
bado umeshangaa, tulia. Eneo la Whangamomona nchini New Zealand, mbuzi
kwa jina Billy Gumboot mwaka 1999 alichaguliwa kuwa rais.
Alikuwa
mnyama wa kwanza kuchaguliwa katika wilaya hiyo lakini hakuwa wa
mwisho, baada yake kuondoka madarakani, mrithi wake alikuwa mbwa aina ya
Poodle aliyepewa jina Tai. Kwa sasa eneo hilo linaongozwa na rais wa kwanza mwanamke, Vicki Pratt.
5. Sokwe wa Rio de Janeiro Sokwe
kwa jina Tiao alipata kura nyingi, ingawa hazikutosha kabisa kumfanya
meya wa mji wa Rio de Janeiro. Kauli mbiu yake ilikuwa: "Mpigie kura
tumbili - upate tumbili." Lakini alipata sanamu.
Sanamu ya Tiao
6. Penguini brigadia Penguini
kwa jina Nils Olav alipewa hata cheo cha Brigadia katika jeshi la
Norway, na hata akakubaliwa kutekeleza majukumu rasmi, mfano kukagua
gwaride.
Hauhitaji Media PlayerPata usaidizi kuhusu Media PlayerBonyeza 'Enter' kuendelea au kurejea mwanzoni
COMMENT AND SHARE...........,
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!