Wanawake, Msing`ang`anie Wanaume Ambao Hawawataki:;
Zaidi ya watu wa 5 wameshakueleza kwamba jamaa hana time na wewe na
ameshachumbia mtu mwingine hukuamini. Mungu sio Mwigulu Nchemba, siku 1
akiwa kwenye mishemishe za kuchepuka simu yake ikajipiga ukamsikia
anaongea na msichana mwingine na baada ya muda ukawasikia wanapiga
kwinchi kwinchi Live wakati alikuaga muda huo yuko kwenye kikao cha
harusi. Mungu akaamua kukuonyesha kitu live.
Ulipomuuliza akaruka futi elfu 6 kwamba unamsingizia una kila ushahidi
kwamba huyo jamaa ni kimeo ila kwa sababu akili yako ina ujibwa ulezi
uliochanganywa na alizeti ukamsamehe, sasa leo amekuoa na tabia zilezile
walizokuonya rafiki zako zimeendelea, unashinda unalia na kuimba Pambio
la bwana tenda miujiza usiaache mpaka mwaka huu upite.
Alishatenda muujiza kukuonyesha ushahidi hukutaka kumsikia, ukapenda
zaidi matarumbeta ya harusi bila kujali ndoa itakuwaje. Pole hakuna
muujiza hapo, jipigie matarumbeta kwa kujitendea muujiza. Kamwe
usidharau Mungu akikuonyesha (clear Signs) kwamba mtu uliyenaye ni
shida. Using'ang'anie kuwa mjumbe wa bunge la katiba kama unahisi posho
haitoshi achia ngazi.
Heri ukose harusi leo ujiandae kwa ndoa bora ya keshokutwa.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!