Wanasayansi wamethibitisha kwamba aina ya kunguru mwitu kutoka New Caledonia kusini mwa Pacific wanaweza kutengeneza zana.
Ndege hao walichunguzwa walipokua wakitumia midomo yao kuchukora chakula kilichokua kimefichwa kati kati ya mbao.
Awali ujuzi huu ullibainika kwa ndege wanaotunza kwenye maabara .
matokeo
ya uchunguzi uliochapishwa kwenye jarida la Open Science, yanasema
kuwa kipaji hiki ni sehemu ya tabia asilia ya ndege.
Mwaka 2002, kunguru mwitu anaetunzwa kwenye maabara ya New Caledonian crow - kwa jina Betty - aliwashangaza wanasayansi.
Watafiti katika chuo kikuu cha Oxford walimpatia chakula katika kikapu kisichoweza kufikiwa kwa urahisi.
Kukifikia
, ndege huyo alipindisha kipande cha waya hadi ndani ya kikapu. Ilikua
ni mara ya kwanza kwa ujuzi huo wa kutengeneza kifaa kuwahi kushuhudiwa
katika ulimwengu wa wanyama.
Betty alikufa mwaka 2005, lakini
baada ya miaka, hatimae uchunguzi ulifanikiwa kurudiwa katika ndege
mwingine alieko kwenye maabara.
Mkuu wa uchunguzi huo Dr
Christian Rutz, kutoka chuo kikuu cha St Andrews cha Scotland, anasema :
"ilionekana ni kama ni kitu ambacho ndege yule alikivumbua katika
maabara ."
Wakati inafahamika kwa muda mrefu kwamba kunguru wa
porini huweza kudonoa vitu kutoka kwenye sehemu zilizojificha za ndani ,
watafiti sasa wamebaini kuwa wanaweza pia kupindisha vijiti sawsa na
wenzao wa maabara.
Katika msururu wa uchunguzi , watafiti waliwakamata kunguru kutoka
misitu ya New Caledonia, na kuwaweka kwa muda mfupi katika viota vya
muda
Dr Rutz anasema: "Hii inamaanisha kwamba tunaweza
kuwafanyia majaribio katika hali ya uchunguzi unaodhibitiwa zaidi -
lakini aina za vipimo tunavyofanya pale, havionyeshi vema namna ndege
hawa walivuyo na akili , wanauliza ni aina gani ya kifaa ambacho
wanakielezea kwa tabia asilia.
Kunguru walipewa vijiti , ambavyo vilikua na ladha ya chakula ambavyo viliwekwa kwenye mashimo kwenye sakafu
"Kitu
kimoja tu tulichowapatia ulikua ni mmea ambao tulifahamu kwa kawaida
wanatumia kutengenezea kifaa mwituni ," alieleza Dr Rutz.
"kwa hiyo kazi ilikua rahisi sana , tuliomnba ndege wetu watengeneze vifaa kisha tuvitumie kutoa chakula kilichofichwa ."
Kunguru hawakuhitaji vijiti maridadi kuchukua chakula , lakini 10 kati ya 18 wa mwituni walifanya hivyo.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!