
NAIBU
Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Selemani Jaffo, amesema Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, ina
wanafunzi hewa 4445 ambao wanasoma katika shule za sekondari za serikali
kinyume na utaratibu.
Jaffo aliyasema hayo wakati akizungumza
na Watumishi wa Halmashauri za Msalala na Mji, juzi, katika ziara ya
kushitukiza, ambapo aliwaasa kufanya kazi kwa weledi kwa kufuata sheria
na taratibu za kuwahudumia wananchi.
Alisema kuwepo kwa idadi
hiyo kubwa ya wanafunzi hewa katika shule za sekondari kunatokana na
maofisa elimu kutokujua takwimu za wanafunzi na kuongeza kuwa, muda
mwingi wamekuwa wakikaa ofisini bila ya kutembelea maeneo ya kazi.
Naibu
Waziri huyo alisema, takwimu za utengenezaji wa madawati, zimekuwa
kinyume na ilivyotarajiwa, hali ambayo imesababisha kuchelewa kumalizika
kama iliovyokuwa imepangwa na Rais John Magufuli.
Pamoja na
mambo mengine, Naibu Waziri huyo aliwaonya watumishi hao kutotumia fedha
vibaya zitakazotolewa na wizara hiyo, kwa ajili ya kutengeneza
miundombinu ya barabara katika halmashauri ya mji wa Kahama.
Mbunge
wa Jimbo la Kahama, Jumanne Kishimba alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa
Halmashauri ya Mji wa Kahama, ina changamoto nyingi zikiwamo za
miundombinu ya barabara, kuzidiwa kwa wagonjwa wanaotoka katika wilaya
16 katika hospitali ya halmashauri ya mji pamoja na upungufu wa
watumishi.
Alisema Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama,
imezidiwa na wagonjwa ambao wanatoka katika sehemu mbalimbali zilizopo
jirani, hali ambayo watumishi wake wanapata wakati mgumu katika kutoa
huduma na wakati mwingine kushindwa kutoa huduma kwa wakati.
COMMENT AND SHARE................................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!