Wakulima wa korosho LIWALE washauriwa kufungua akaunti za benki:;
Wakulima wa zao la korosho wilayani LIWALE mkoani LINDI wametakiwa
kufungua akaunti kwa ajili ya kupitishia malipo ya fedha za mauzo ya
korosho
Mwenyekiti wa chama cha ushirika cha msingi Umoja, HASSANI MPAKO
amesema utaratibu huo uliyotolewa na serikali ni hatua ya kudhibiti wizi
wa fedha za wakulima unaofanywa na majambazi na baadhi ya watendaji wa
vyama vya ushirika wasiokuwa waaminifu kuwaibia wakulima.
MPAKO amesema utaratibu wa kufungua akaunti benki na kujiunga na
Vyama vya akiba na mikopo Saccos kwa ajili ya kupitishiwa malipo ya
fedha zao umekuja baada ya wakulima kulalamika kuwa wanakosa malipo
stahiki kutokana na wizi unaofanywa na majambazi kupora fedha za
wakulima .
Baadhi ya wakulima wa korosho wilayani LiWALE wameipongeza serikali
kwa hatua hiyo itakayomsaidia mkulima kupata malipo yake kwa uhakika.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!