Wajumbe 8 wa kundi la WhatsApp wametiwa mbaroni Burundi:;
Polisi nchini Burundi wamewatia
nguvuni wajumbe wanane wa mtandao wa kijamii wa WhatApp . Kulingana na
msemaji wa wizara ya usalama wa umma nchini humo Pierre Nkurikiye watu
hao ambao ni wakazi wa mji mkuu Bujumbura walikamatwa mnamo tarehe 20
Agosti kutokana na "vitendo vya uhalifu wa kimtandao ".
Wanane hao kwa pamoja walikuwa ni wajumbe wa kundi moja la WhatsApp.
Kwa
mujibu wa Nkurikiye WhatsApp mijadala inayoendelea katika makundi ya
WhatsApp inaeneza taarifa za "matusi ni chanzo cha ghasia nchini humo
hasa wakati wa hali ya sintofahamu".
Mkuu wa uchunguzi wa habari
Innocent Muhozi ameishutumu serikali kwa kujaribu " kukamilisha njama
yake ya kuzima uhuru wa mawasiliano" waliyoianzisha kwa kuwakamata
watumiaji wa WhatsApp.
Muhozi anasema mtandao huo ulikua ndio chanzo cha taarifa huru kilichobaki kwa warundi .
Wakazi
wa Bujumbura hutumia WhatsApp kila siku kama mfumo wa kutoa tahadhari
baina yao kuhusu utekeji nyara, kamata kamata ya maafisa wa usalama na
kutoweka na matukio ya uhalifu.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!