Wanamichezo wa mazoezi ya viungo
kutoka Korea Kusini na Kaskazini, ambao wanashiriki Michezo ya Olimpiki
Rio 2016, wameuonesha ulimwengu ishara ya umoja, kwa kupiga selfie
pamoja.
Lee Eun-ju wa Korea Kusini na Hong Un-jong wa Kaskazini
walipiga picha wakiwa wametabasamu wakati wa mazoezi kabla ya kuanza kwa
michezo hiyo.
Picha za wanawake hao wawili zimesifiwa sana kwa kuashiria moyo wa Olimpiki wa kuwaleta watu pamoja.
Korea Kaskazini na Kusini huwa na uhasama mkubwa.
Uhusiano baina ya nchi hizo mbili umedorora hata zaidi, kutokana na hatua ya karibuni ya Pyongyang kufanyia majaribio makombora.
Picha bora zaidi Olimpiki?
"Hii
ndiyo maana huwa twashiriki Olimpiki," mchanganuzi wa masuala ya
kisiasa Ian Bremmer aliandika kwenye Twitter na kuweka picha hiyo.
Ujumbe wake ulisambazwa zaidi ya mara 18,000.
Wengine hata hivyo hawakufurahishwa na hilo.
"Anaruhusiwa
kufanya urafiki na adui?", mmoja wa watu mitandaoni waliuliza, na
wengine wakaeleza wasiwasi kwamba huenda Hong akaadhibiwa akirejea
nyumbani.
Lee, 17, na Hong, 27, wote walishiriki kama wachezaji wa
kufuzu wakiwa binafsi. Ilikuwa mara ya kwanza kwa Lee kushiriki michezo
ya Olimpiki.

Wengi walieleza tofauti iliyopo baina ya wanawake hao wawili na timu ya
Olimpiki ya Lebanon iliyokataa kuabiri basi moja na wanamichezo wa
Israel.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!