Usain Bolt ashinda dhahabu yake ya tatu Rio:;
Mwanariadha wa kasi zaidi duniani mzaliwa na Jamaica Usain Bolt
amepata dhahabu katika mbio tatu tofauti katike kile kinachojulikana
katika kiingereza kama "trible trible" au tatu tatu.
Shindano lake la mwisho lilikuwa la mita 100 kupokezana vijiti mara nne.
Alipokea
kijiti mwisho katika timu yake na akafululiza kishujaa na kumshinda
mpinzani wake wa karibu kutoka Japan, aliyeshinda Marekani na kuchukua
Shaba.
Bolt ameshinda dhahabu mara tatu katika Olimpiki zote tatu
alizoshiriki ndipo ushindi wake huu ukatambuliwa kama trible trible
yaani tatu tatu.
Bolt mwenye umri wa miaka 29, alishinda dhahabu katika mbio za mita
100 na 200 mjini Rio na ndiye mwanariadha wa kwanza kushinda mbio tatu
katika mashindano matatu ya olimpiki
Awali timu ya marekani ya wanawake ilishinda mbio sawa na hizo za kupokezana vijiti.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!