UKWELI KUHUSU BANGI:;
Bangi ni neno ambalo hutumika
kuelelezea sehemu iliyokaushwa ya maua, mbegu, mche na majani ya mmea
ujulikanao kama Indian hemp. Uko
mitaani bangi ina majina mengi na watumiaji wake wameipa majina kama: dope, nyasi, majani, mche, ganja, magugu, kitu,
sigara kali, blanti na mboga.
Kwa kitaalam “
cannabis” huelezea aina mbali mbali za
dawa za kulevya zitokanazo na mmea wa
Indian
hemp ambazo ni bangi (
marijuana)
na
hashish.
Aina hizi za dawa zitokanazo na
mmea huu ziko katika kundi la dawa za kulevya ziletazo maruweruwe
(hallucinogen) au dawa zinazoathiri
ubongo na kubadili jinsi tunavyotazama mambo katika uhalisia wake.Kuna zaidi ya
aina 400 za kemikali katika mmea huu na kemikali ya kulaumiwa inayohusika na
mabadiliko haya katika ubongo hujulikana kama tetrahydrocannabinol (THC). Kiasi cha THC hutofautiana kulingana
na eneo ulikolimwa mmea wa Indian hemp.
Kama tulivyoona bangi ni sehemu
iliyokaushwa ya majani, mbegu,maua, na mche na huwa na rangi ya kijani,kijivu
au brauni na bangi ni dawa ya kulevya ambayo hutumika kinyume cha sheria katika
sehemu nyingi duniani.
Bangi hutumika kwa kuvuta moshi
kutoka katika msokoto, sigara iliyoungwa au bomba maalum ya kuvutia moshi wake.
Ni mara chache huchanganywa katika chakula, kuliwa kama mboga au kutengeneza
kinywaji. Wakati mwingine watumiaji hupukutisha sigara na kujaza bomba la
sigara bangi au bangi iliyochanganywa na dawa nyingine za kulevya kama cocaine na aina hii hujulikana na
watumiaji kama “blunt”
Mtumiaji anapovuta msokoto wa bangi, huanza kufanya kazi baada ya dakika chache na mvutaji huanza kuhisi mapigo ya
moyo yakienda mbio, mapokeo ya uhalisia huanza kubadilika na kuona vitu visivyo
katika uhalisia (ndoto za mchana/maruweruwe).Matokeo
haya ya muda mfupi baada kuvuta moshi wa bangi, huweza kudumu kwa muda wa saa
mbili hadi nne au kuendelea kwa muda mrefu zaidi ikitegemea na kiasi cha THC
kilichovutwa na ukali wake.
Mara nyingi wavutaji wa bangi
huvuta moshi kwa nguvu ndani ya mapafu na kuushikilia kwa muda mrefu ili kuongeza
ufanyaji kazi wa THC ukilinganisha na anayevuta sigara na hii husababisha
madhara makubwa katika mapafu ya mvutaji. Mbali na maudhi kama kukohoa na koo
kuwasha, imeonekana kuwa uvutaji wa aina hii wa moshi unamweka mvutaji katika
hatari mara tano zaidi ya kupata saratani ukilinganisha na mvutaji sigara.
Matatizo ya ubongo yanayopelekea
kuathiri afya ya akili ni ugonjwa mbaya uwapatao wavutaji wa bangi. Anayevuta
bangi huwa na uwezo mdogo wa kumbukumbu na pia humuondolea uwezo wa asili wa
kufanya maamuzi yaliyo sahihi ukilinganisha na mtu asiyevuta bangi.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!