Ukimya wa TipTop Connection Unaniumiza - Kassim Mganga:;

Msanii Kassim Mganga ambaye awali alikuwa ni moja kati ya wasanii kutoka
katika kundi la Tip Top Connection amesema ukimya wa kundi hilo
unamuumiza na kumgusa sababu yeye bado ni mwanafamilia wa Tip Top
Connection licha ya kutofautiana kibiashara.
Kassim Mganga akiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo alisema yeye bado ni
mwanafamilia wa Tip Top Connection hivyo alikuwa anapenda kuona familia
yake hiyo inaendelea na moto ule ule kama zamani.
“Unajua unapoongelea Tip Top Connection na Kassim Mganga ni kama
familia, hivyo ile ni familia yangu japo tulipishana kwenye masuala ya
biashara tu. Hivyo kama mwanafamilia wa Tip Top Connection ukimya wao
unanigusa na kuniumiza sababu nilikuwa natamani kuona chama linaendelea
na moto ule ule kama zamani” alisema Kassim Mganga
Mbali na hilo Kassim Mganga ameahidi kuja na band yake katika siku
zijazo kwani anatamani kufanya muziki wa live kwenye show zake.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!