Mfumo
wa Apple wa utendaji wa iOS umegundulika ambao utawezesha
kupachikwa kwenye kifaa cha uchunguzi kukiwezesha kubofya kwenye
kiunganishi.
Uvumbuzi huo ulifanyika baada ya wakili anayetetea
haki za kibinadamu kutoa taarifa kwa watafiti wa masuala ya usalama
kuhusu jumbe alizozipata bila kutarajia.
Waligundua taarifa nyingine tatu za awali zisizofahamika zilizovuja kutoka kwa mfumo wa Apple .
tangu wakati huo Apple imetoa taarifa ya kuelezea tatizo hilo na namna linavyoshughulikiwa na kampuni hiyo.
Makampuni
mawili ya usalama yaliyohusika , Citizen Lab na Lookout, yamesema
yamehifadhi taarifa hizo za uvumbuzi hadi suala hilo litakapopatiwa
ufumbuzi.
Kampuni ya Citizen Lab inasema , simu yake ya iPhone 6
ingekuwa ''imefunguliwa'' , ikimaanisha mfumo mwingine ambao
haukuidhinishwa ungelikuwa umewekwa kwenye simu yake.
"Na kama
simu yake ingeathiriwa , ingekuwa kifaa cha upelelezi cha digitali ndani
ya mfuko wake wa nguo, yenye uwezo wa kung'amua taarifa kwa kutumia
kamera na kipaza sauti cha simu kurekodi simu zake za WhatsApp na
Viber , kuingia kwenye jumbe alizotuma kwa simu na kuweza kumfuatilia
kote anakoenda," ilisema kampuni ya Citizen Lab.
"Hatuna taarifa zozote za matukio ya aina hii ya iPhone suala linalofanya tukio hili kuwa la nadra ."
Watafiti
wanasema wanaamini mfumo huu wa uchunguzi unaohusisha spyware
ulibuniwa na kampuni ya NSO Group, ya Israel ya ''vita vya mitandaoni"
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako
COMMENT AND SHARE.....................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!