UBUYU NA FAIDA ZAKE:;
Mbuyu ni jina la Kiswahili la mti
wenye asili ya kale wa jamii ya Adansonia,
na kuna aina tisa katika
jamii ya mibuyu ambapo aina sita zina asili ya
kisiwa cha Madagascar na aina mbili ina asili ya barani Afrika na Ghuba ya
Uajemi na moja ina asili ya bara la Australia. Mti wa mbuyu una uwezo mkubwa wa
kuhifadhi maji, na huifadhi takriban kiasi cha lita 100,000 na kuufanya
mti huu kuweza kukabiliana na hali ya ukame hususan katika maeneo yaliyo na
hali ya ujangwa. Uwezo wa kuhifadhi maji mengi hutokana na mtii huu kupukutisha
majani yake nyakati za kiangazi.
Unga wa ubuyu uliokaushwa wa mti wa jamii ya A digitata huwa na virutubisho vingi kama wanga, protini, Vitamini B2(Riboflavin),Kalshamu,Magnesiamu,Potasiamu, Chuma, Protini muhimu, Vitamini C na aina nyinginezo za
virutubisho.
Jedwali likionyesha kiasi cha virutubisho katika gramu
100 za ubuyu.
Aina ya kirutubisho
|
Kirutubisho
|
Kiwango kilichopo
|
Vitamini
|
Vitamini A
|
0.0µg
|
|
Vitamini B2
|
0.6
|
|
Vitamini E
|
1.0 µg
|
|
Vitamini C
|
201mg
|
|
Thiamine
|
0.0mg
|
|
Niacini
|
3.4mg
|
|
Vitamini B 6
|
0.1mg
|
|
Folic acid
|
13 µg
|
Madini
|
Kalshamu
|
36mg
|
|
Phosphorasi
|
199mg
|
|
Magnesiamu
|
46mg
|
|
Potasiamu
|
1221mg
|
|
Munyu (Sodium)
|
3mg
|
|
Chuma
|
1.9mg
|
|
Zinki
|
0.3mg
|
|
Shaba
|
0.7mg
|
|
Manganizi
|
0.3mg
|
Protini muhimu
|
TRP(Tryptophan)
|
48mg
|
|
THR(Threonine)
|
145mg
|
|
ILE(Isoleucine)
|
145mg
|
|
LEU(Leucine)
|
252mg
|
|
LYS(Lysine)
|
222mg
|
|
MET(Methionine)
|
39mg
|
|
CYS(Cysteine)
|
58mg
|
|
PHE(Phenylalanine)
|
135mg
|
|
TYR(Tyrosine)
|
125mg
|
|
VAL(Valine)
|
204mg
|
|
ARG(Arginine)
|
59mg
|
|
HIS(Histidine)
|
6mg
|
Moja ya umuhimu mkubwa kiafya wa
tunda la ubuyu ni uwezo mkubwa wa kuimarisha kinga ya mwili, kuimarisha mifupa,
kusaidia mfumo wa umeng’enyaji tumboni, kupunguza maumivu na uvimbe na
kusisimua utengenezaji wa seli na tishu mpya . Pia kusaidia kupunguza shinikizo
la damu na kuzuia magonjwa sugu.
Sababu inayolifanya tunda la
mbuyu kuwa la pekee ni kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha virutubisho kama
madini, vitamini na protini. Ubuyu una kiwango kikubwa pia cha madini ya chuma,
ambayo ni sehemu muhimu ya protini ya haemoglobin inayohusika na usafirishaji
wa hewa ya Oxyjeni na protini hii ni sehemu ya seli hai nyekundu ya damu. Ulaji
wa ubuyu waweza kutuepusha na ugonjwa wa kupungukiwa damu ujulikanao kitaalam kama Anemia. Matumizi yake ni pamoja na
kuupatia mwili nishati inayoitajika ili mgonjwa apone haraka.
Kiwango kikubwa cha madini ya
Potasiamu katika tunda la ubuyu, kunapelekea tunda hili kuwa na manufaa
kwa afya ya moyo. Madini ya Potasiamu husaidia kutanua mishipa ya damu na
ateri, na matokeo yake huusadia kuupunguzia moyo kutumia nguvu nyingi katika
kusukuma damu . Kutanuka kwa mishipa ya damu kutapunguza shinikizo la damu kwa
hiyo kutatuepusha na magonjwa ya moyo
yakiwemo yale ya kukakamaa kwa mishipa ya damu, shambulizi la moyo na magonjwa
mengine ya moyo yaliyo hatari.
Uimarishwaji wa mifupa kutokana
na ubuyu ni dhahiri kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha madini ya Kalshamu na
Magnesiamu. Kama una wasiwasi wa udhoofu wa mifupa kutokana na umri mkubwa,
waweza kuongeza ubuyu katika orodha ya lishe yako kwani itakusaidia kuimarisha
mifupa unapoelekea uzeeni. Kwa watoto madini haya ni muhimu kwa kuwa huimarisha
mifupa na meno, na yatawaepusha na ugonjwa wa kupinda mifupa ujulikanao kama Rickets.
Ubuyu una aina mbili za fiba (nyuzi lishe), zile zinazochanganyika na
maji na zisizo changanyika na maji, na hii ndio sababu ubuyu umekuwa ukitumika
kwa miongo mingi kusaidia kurekebisha mmeng’enyo wa chakula tumboni na kuondoa
maumivu yasababishwayo na matatizo ya
mmeng’enyo. Fiba hizi husaidia pia kurekebisha kiwango cha sukari katika damu,
kiwango cha lehemu na kuboresha afya ya moyo. Fiba pia husaidia kurekebisha
kiwango cha bacteria wenye faida tumboni na kuboresha mmeng’enyo.
Viondoa sumu(Anti-oxidant) vimesheheni katika ubuyu, na hii inamaanisha kuwa
tunda hili husaidia kutukinga na aina nyingi za magonjwa pamoja na saratani.
Vitamini C ni aina ambayo hupatikana
kwa wingi katika ubuyu, na uimarishwaji wa kinga ya mwili hutokana na kuwepo
kwa vitamini C(Ascorbic acid)kwa
wingi. Kwa hiyo ubuyu husaidia kuongezeka kwa seli hai nyeupe za damu na
kusisimua kinga ya mwili kupambana na vijimelea vya magonjwa.
Vitamini C pia husaidia katika
utengenezaji wa Kollajeni(Collagen),
protini ambayo husaidia kukarabati seli, tishu, mishipa ya damu na mifupa. Kiwango
kikubwa cha Vitamini C sio tu kwamba huimarisha kinga ya mwili, bali huusaidia
mwili kuwa na utendaji kazi bora wa mifumo mbalimbali i na hupelekea kupona
haraka kwa magonjwa, majeraha hata kwa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji.
Nchini Tanzania kabila la
wasandawe hutumia unga wa ubuyu katika uchachushaji wa juisi ya miwa
kutengeneza bia na majani yake hutumiwa kama mboga.Unga wake hutumika na watu
wengi kutengeneza juisi yenye ladha ya kuvutia. Pia ubuyu huliwa kwa kumung’unya
mbegu zake hususan na watoto na kina mama.
Nchini Zimbabwe unga wa ubuyu
hutumika kutengeneza chakula cha asili pamoja na kuchanganya kwenye uji ili
kuongeza ladha.Nchini Malawi wakina mama wameanzisha ujasiriamali wa uvunaji wa
ubuyu kwa ajili ya biashara na hujipatia kipato kinachowasaidia kulipa ada za
shule za watoto.
Tahadhari
Mafuta ya mbegu za tunda la mbuyu yaweza kuwa na kiwango kikubwa cha
kemikali ijulikanayo kama
Cyclopropenoid
fatty acids (CPFA), ambayo katika tafiti nyingi imeonekana kusababisha
ugonjwa wa ini na hata saratani. Pia ni vyema kuhakikisha unga wa ubuyu
unaandaliwa katika mazingira au hali ya usafi ili kuepuka maambukizi ya
magonjwa.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!