Ubishoo Kwenye Muziki Niliuanzisha mimi - Mr Blue:;

Mr Blue
Mkali wa wimbo ‘Mboga Saba’ Mr Blue amesema yeye ana mchango mkubwa katika mabadiliko ya muziki wa bongofleva nchini.
Akiongea katika kipindi cha Ndoto Kubwa cha Clouds TV Jumapili hii, Mr
Blue amesema yeye ndiye msanii wa kwanza kufanya muziki akiwa na swagga.
“Mimi baada ya kuingia kwenye muziki kuna vitu ambavyo nilivifanya mimi
kama mimi ili kuonyesha utofauti, kuanzia kwenye kuvaa, swagga za
kuimba, kutoboa masikio. Kwa hiyo hivyo vyote kwa wakati ule watu
walikuwa wananiona huyu jamaa vipi, kumbe mimi tayari nilikuwa
nimeshaiona future, ndio maana wasanii wengi waofanya muziki kwa swagga,
utasikia ana flow kama Mr Blue, tayari tulishaacha alama huko ndiyo
maana tunaendelea kufanishwa,”
Katika hatua nyingine Blue amesema yeye alikuwa anapenda kusoma kuliko
kufanya muziki, lakini akaamua kujifunza kufanya muziki mpaka akaweza.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!