Tatizo la Nguvu za Kiume na Suluhisho lake:;
Makala hii ni maalumu kwa ajili ya wanandoa tu na si vinginevyo au
kama elimu kwa wanandoa watarajiwa. Muogope Mungu uzinzi ni dhambi kubwa
sana.
Katika kilele cha juu kabisa cha furaha katika ndoa, kama
inavyojulikana, ni sherehe inayopatikana katika tendo lenyewe la ndoa.
Ingawa, ili furaha hiyo ipatikane ni lazima tendo hilo liwe limefanyika
katika hali ya afya kwa wanandoa wote wawili.
Nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha
‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’. Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine. Inaweza kuwa ni hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.
Pamoja na hayo yote, elimu mhimu ambayo mwanaume anatakiwa kuwa nayo,
ni kuwa nguvu za kiume hazipatikani kwa kutumia madawa ya kemikali au
mahala pengine; bali zinatokana na vyakula tunavyokula kila siku.
Sababu za Wanaume kuishiwa nguvu za kiume:
Kuishiwa nguvu za kiume ni jambo la kawaida kwa wanaume wengi. Ni
kushindwa kwa uume kudumu kusimama barabara kwa ajili ya tendo la ndoa,
au kuwahi kufika kileleni.
Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka sababu ya umri.
Tafiti mbalimbali zinasema wanaume wa umri kuanzia miaka 61 na kuendelea
ndiyo wanapatwa na tatizo hili zaidi kuliko wanaume wenye umri wa miaka
41 Kushuka chini.
Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndio
wanaokabiliwa sana na tatizo hili. Hii ni kutokana na kwamba wengi wao
wanakuwa hawaelewi aina ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, namna wanavyotakiwa kuishi ili kupunguza janga hilo, wanakunywa pombe na hawajishughulishi na mazoezi ya viungo. Mazoezi ya viungo hupunguza tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kwa asilimia kubwa sana.
Kupungukiwa nguvu za kiume kunaweza pia kuwa kumetokana na mambo ya kihisia, kwa kiingereza
‘emotional causes’. Vitu vingine vinavyoweza kusababisha kupungua kwa
nguvu za kiume ni pamoja na magonjwa kama vile ugonjwa wa Kisukari na
Shinikizo la juu la damu.
Asilimia 51 mpaka 61 ya wanaume wanaosumbuliwa na kisukari wanapatwa
na tatizo la uume kushindwa kusimama vizuri. Kadharika wagonjwa wa
kiharusi na wale waliotekwa na ulevi nao ni miongoni mwa watu wanaoweza
kupatwa kirahisi na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Walevi wengi
wa pombe kwa mfano wanakabiliwa na tatizo la uzalishaji mchache wa mbegu
za kiume (manii).
Wengine wenye hatari ya kupatwa na tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume ni pamoja na wanaume wenye
shinikizo la juu la damu, wenye matatizo ya tezi, waliowahi kufanya upasuaji katika viungo vya uzazi
wakabaki na majeraha, watu wanaotumia dawa zenye kemikali kiholela bila
kushauriwa na wataalamu na wale wanaougua maradhi yanayodhoofisha
msukumo wa damu kwenda katika mishipa ya uume.
Pamoja na hayo, tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linaweza kutibika kwa watu wa rika zote.
Kabla dakatari hajaanza kukutibu tatizo kupungukiwa nguvu za kiume, atataka kujuwa:
- Umri wako
- Utendaji wa tendo la ndoa kabla na baada ya kuugua
- Afya yako kwa ujumla
- Matatizo katika ndoa ikiwa kuna ugomvi wowote n.k
- Nini sababu ya wewe kutaka kupona
Kuwa na mtaalamu mzuri ni njia ya kwanza katika kupata uponyaji
sahihi. Ni mhimu wewe kujisikia vizuri na kuwa na imani na daktari wako.
Kwa kufanya hivi utakuwa umepiga hatua nzuri kelekea kwenye ufumbuzi wa
tatizo lako.
Nini Sababu ya uume kushindwa kusimama?
Kushindwa kwa uume kusimama pia hutambulika kama kuishiwa nguvu za
kiume. Ni kitendo cha mtu kushindwa kusimamisha uume au kudumisha
usimamaji wa uume kwa muda wa kutosha kufanya tendo la tendo na mwenza
wake. Pamoja na ukweli kuwa mara zote Mwanaume lazima atafika kileleni,
hali huweza kuwa tofauti kwa upande wa pili kwani mwanamke anahitaji
mwanaume akawie zaidi ili na yeye (mwanamke) aweze kutosheka.
Mkeo hupendelea ukawie na ikiwezekana ukawie zaidi. Kama utakuwa unawahi kumaliza, basi mkeo anakuwa hapati raha kamili.
Ingawa, kama una tatizo la kuwahi kufika kileleni hauko peke yako.
Asilimia 30 hadi 40 ya wanaume wa rika zote wanakabiliwa na tatizo la
kuwahi kufika kileleni au kupungukiwa kwa nguvu za kiume. Hata hivyo
kutambuwa tu kwamba wanaume wengine pia wana tatizo kama lako siyo
sababu ya wewe kukaa tu bila kutafuta suluhisho la tatizo lako.
Habari njema ni kuwa zipo njia zinazoweza kuleta matokeo mazuri na
hatimaye kulimaliza tatizo hili bila madhara mabaya hapo baadaye.
Wakati mwingine uume kushindwa kusimama inaweza kuwa si tatizo,
lakiini jambo hilo linapojitokeza kila mara na kwa kipindi kirefu
inaweza kuleta msongo wa mawazo kwa mume na hata kwa mke. Sababu
nyingine amabzo zinaweza kupelekea uume usisimame vizuri ni pamoja na
matatizo ya mhemko kama;
- Wasiwasi
- Hasira
- Msongo wa mawazo (Stress)
- Huzuni
- Hofu na mashaka
- Kukosa hamu ya tendo la ndoa n.k
Ili uume usimame vizuri ni lazima:
- Mfumo wako wa neva uwe na afya nzuri inayopelekea mpwito neva (nerve impulses) katika ubongo, uti wa mgongo na uume.
- Mishipa ya ateri iliyo na afya ya ndani na iliyo karibu na corpora cavernosa
- Misuli laini yenye afya na tishu za ufumwele (fibrous tissues) ndani ya corpora cavernosa
- Kiwango sahihi cha oksidi nitriki (nitric oxide) ndani ya uume.
Uume kshindwa kusimama vizuri kunaweza kusababishwa pia kama
kipengele kimojawapo hapo juu hakifanyi kazi vizuri. Mambo mengine
yanayopelekea kupunguwa kwa nguvu za kiume, uume kushindwa kusimama
vizuri na kuwahi kufika kileleni ni:
- Uzee
- Kisukari
- Kujichua/Punyeto
- Uzinzi
- Kukosa Elimu ya vyakula
- Kutokujishughulisha na mazoezi
- Shinikizo la juu la damu
- Ugonjwa wa moyo
- Uvutaji sigara/tumbaku
- Utumiaji uliozidi wa kafeina. Na kama hujuwi kafeina ni kitu gani.
- Kudhurika kwa neva au uti wa mgongo
- Madawa ya kulevya
- Kupungua kwa homoni ya testerone
- Athari kutoka kwa baadhi ya dawa
- Pombe
Nguvu za kiume na mzunguko wa damu:
Kitu gani husababisha uume usimame?
Unaweza kujibu ni
msisimko. Ni kweli, Jibu lako linaweza kuwa sahihi.
Hata hivyo msisimko ni matokeo. Kipo
kinachosababisha kutokea huo msisimko. Bila hicho, hakuna msisimko unaoweza kutokea.
Kila mwanaume anatakiwa kujuwa jibu sahihi la swali hili ili
atakapopatwa na tatizo atambuwe wapi pa kuanzia na pa kuishia. Siyo
lazima uwe daktari, Elimu ya kutambua mfumo wako wa mwili unavyofanya
kazi ni mhimu sana kwa kila mtu na si kwa madaktari pekee kama watu
wengi mnavyodhani.
Kutokusoma soma lolote kuhusu miili yetu inavyofanya kazi ndiyo
sababu kubwa inayotufanya kuparamia dawa kiholela na hivyo kujikuta
tunapata madhara zaidi badala ya kujitibu.
Mzunguko wa damu ndicho kitu kinachofanya uume USIMAME. Na kabla hujaendelea kusoma tambua jambo moja mhimu; ‘’Asilimia 94 ya damu ni maji’’. Hii ni kusema katika kila lita 10 za damu, lita 9 kati ya hizo 10 ni maji. Kwa kifupi maji ndiyo kila kitu mwilini, nakushauri upendelee Kunywa maji bila KUSUBIRI KIU.
Mzunguko wa damu unaofanya kazi vizuri kama inavyotakiwa na usio na
hitilafu yeyote ni kipengele mhimu sana katika afya ya mwili, mishipa na
kusimama kwa uume wako.
Kwanini mzunguko wa damu ni mhimu?
Mzunguko wa damu wenye afya bora husambaza damu ya kutosha katika
viungo vyote vya mwili ikijumuisha pia damu iliyo katika mishipa ya
uume. Hivyo, hata kama utagusana na mwanamke hautaweza kufanya lolote
ikiwa damu haizunguki katika viungo vyako kama inavyotakiwa. Mtazame mtu
aliyekufa, damu yake haizunguki, je anaweza kufanya lolote? Hata hivyo
huo ni mfano mkubwa sana.
Hii ni kusema kuwa, chochote ambacho kinazuia mtiririko wa damu
kwenda kwenye uume kinaweza kuzuia kusimama kwa uume. Kama mishipa ya
vena na ateri imeziba, mwili wako hautaweza kusimamisha uume vizuri. Hii
ni kutokana na kwamba uume hautapata damu ya kutosha.
Mara nyingi vena zilizoziba kutokana na mzunguko dhaifu wa damu ni
sababu ya kushindwa kusimama uume kwa wanaume wengi wenye miaka 60
kwenda juu, wanaume wenye kisukari na pia wanaume wenye hali ya kukauka
kwa vijiateri vya ateri, na wenye maradhi ya moyo.
Baadhi ya wanaume wanapatwa na tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kama
matokeo ya kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo yanaweza kuzuia
mtiririko mzuri wa damu kwenye uume. Inashauriwa pia kuepuka vinywaji na
vyakula ambavyo husindikwa viwandani.
Katika tendo la ndoa kwa mwanaume, mishipa ya damu ya ateri ina
nafasi kubwa sana sababu ya kazi yake ya usafirishaji wa damu kwenda
sehemu mbalimbali za mwili, hivyo unashauriwa kujifunza namna ya kutunza
ateri za mwili wako ili kuruhusu mtiririko mzuri wa damu mwilini mwako.
Pia ni mhimu sana kuwaona wataalamu wa tiba kuhusu unavyojisikia na
jinsi unavyohisi kuwa pengine unaweza kuwa na tatizo katika mishipa yako
ya ateri. Jaribu kujiwekea utaratibu wa kujichunguza afya yako mara kwa
mara kama utahisi kunyemelewa na tatizo hili. Baadhi ya watu hufanya
maradhi kuwa sugu kwa sababu ya kuacha kujichunguza mara kwa mara hadi
wauguwe, huku ni kukosa kuelewa na kushindwa kujithamini na kujipenda
mwenyewe.
Jitibu tatizo la kupungua nguvu za kiume
Katika kujitibu tatizo hili jambo la kwanza ni kuelewa ni nini kimesababisha tatizo hilo kwa upande wako.
Njia 13 za kujitibu tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume:
1. Acha mawazo
Mawazo na mfadhaiko huondoa mtiririko mzuri wa damu kwenda kwenye uume na kusababisha nguvu kupungua nguvu za kiume na hata uume wenyewe.
Ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko au stress uangalifu mkubwa
unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote. Katika hali ya
mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano,
wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale
kama mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba kwa
Mungu huenda akaenda kukutangaza kwa majirani!.
Utajuwaje kama una msongo wa mawazo au stress? ili kujuwa kama una stress au hauna.
2. Jitibu magonjwa yafuatayo
Kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, vidonda vya tumbo, shinikizo la juu la damu au uzito kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza maradhi haya. Tatizo ni kuwa watu wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo ambalo si kweli.
Kisukari, shinikizo la juu la damu, vidonda vya tumbo na hata uzito
kupita kiasi ni magonjwa yanayotibika kabisa hasa kwa kutumia dawa
mbadala na kufuata muongozo sahihi katika kula na kunywa kwa kipindi cha
majuma kadhaa.
3. Acha vilevi
Kama tatizo linatokana na matumizi ya vilevi, hatua ya kwanza ni
kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha kwanza, unatakiwa ujiulize
mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo vilevi? Mtu anayejali
vilevi kuliko hata afya yake hafai.
Kuna watu wanajidanganya kwamba ukitumia sijuwi kilevi fulani nguvu
zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo mwanzoni mwa matumizi ya hicho
kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo utakavyoendelea kuwa
mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata hicho kilevi hakitasaidia
kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika tatizo lako
itakapojitokeza.
4. Fanya mazoezi ya viungo
Zingatia sana umhimu wa
mazoezi ya viungo. Bila kujishughulisha na
mazoezi ya viungo kila siku itakuwa ni vigumu sana kwako kupona tatizo la
upungufu wa nguvu za kiume.
Kutengeneza mishipa na kupunguza uzito
isiwe ndiyo sababu pekee ya kwenda gym. Kama unahitaji nguvu za kiume
na uume wenye afya, unahitaji kujishughulisha na mazoezi ya viungo mara
kwa mara ili kusafisha mishipa ya damu na hivyo kuongeza kiasi cha
utiririkaji wa damu kwenda kwenye uume.
Kama uzito wako upo juu sana na ni mnene fanya mazoezi ya kukimbia (jogging) kila siku kwa mwezi mmoja mpaka miwili.
Kama uzito wako upo sahihi tu kwa mjibu wa urefu wako
fanya sana mazoezi ya kuchuchumaa na kusimama. Una chuchumaa na
kusimama mara 25 mpaka 30, unaweza kupumzika dakika mbili unaendelea
tena kuchuchumaa na kusimama hivyo hivyo unapumzika dakika 2 mpaka
mizunguko (rounds) mitano kila siku.
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!