BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU SABABU ZA KUTOKUCHAGULIWA KWA BAADHI YA WALIOOMBA KUDAHILIWA
KATIKA KOZI ZA CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017
Baraza linapenda kuwaarifu wote
walioomba kudahiliwa katika kozi za cheti na diploma na umma kwa ujumla
kuwa kuna baadhi ya waombaji ambao hawakuchaguliwa kwenye uteuzi wa
kwanza ambao ulitolewa tarehe 22 Julai 2016.
Mwombaji ambae hakuchaguliwa hupaswa
kuangalia kwenye kurasa yake binafsi (profile) ili kupata sababu za
kutokuchaguliwa. Sababu za kutokuchaguliwa zinaweza zikawa kama
ifuatavyo:
1. Sifa za muombaji kuwa pungufu kulinganisha na sifa za chini za kozi;
2. Nafasi za mafunzo katika chuo na kozi husika kujaa kutokana na ushindani wa waombaji wenye sifa za juu zaidi.
3. Kutokamilisha ujazaji wa maombi kwenye mfumo;
4. Kutoambatanisha vyeti vya masomo kwa baadhi ya waombaji; na
Waombaji wanashauriwa kusoma kwa
makini sababu hizo na kufuata ushauri unaotolewa ili kuweza kuchaguliwa
katika uteuzi unaofuata.
Baraza linaomba ifahamike kuwa vyuo na
kozi zilizojaa hazitaonekana tena wakati wa maombi bali kozi
zitakazoonekana ni zile zenye nafasi tu. Orodha ya kozi zilizojaa
zimeainishwa hapa Baraza pia linapenda kuwaarifu
waombaji waliofanya maombi kwenye vyuo vya Ualimu vya Serikali kuwa
uteuzi kwenye vyuo hivyo unasubiri mwongozo wa Serikali na hivyo
watafahamishwa punde uteuzi utakapokamilika. Waombaji wa vyuo hivi
wanashauriwa kusubiri na kutokubadili machaguo yao hadi kutangazwa kwa
uteuzi kwa vyuo vya Ualimu vya Serikali.
Aidha Baraza linapenda kuwafahamisha
waombaji wa Shahada ya Kwanza waliofanya maombi kupitia mfumo wa pamoja
wa udahili wa Baraza kuwa utaratibu wa kukamilisha maombi yao utatolewa
baada ya mashauriano kati ya Baraza na Tume ya Vyuo Vikuu
yatakapokamilika.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
Tarehe: 28 Julai, 2016
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!