Baraza
linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi za cheti na
diploma na umma kwa ujumla kuwa muda wa nyongeza wa kutuma maombi kwa
mwaka 2016/2017 umeongezwa hadi tarehe 13 Agosti 2016 ili kuruhusu ambao hawakukamilisha maombi yao kuyamaliza na ambao hawajafanikiwa kuomba kutuma maombi yao.
Baraza linaomba ifahamike kuwa vyuo na
kozi zilizojaa hazitaonekana tena wakati wa maombi bali kozi
zitakazoonekana ni zile zenye nafasi tu pia baraza linashauri waombaji
wajipime na kuangali ushindani wa kozi ili kufanikisha kuchaguliwa kwao.
Vyuo na kozi zilizo na nafasi zimeainishwa hapa.
Baraza pia linapenda kuwaarifu
waombaji waliofanya maombi kwenye vyuo vya Ualimu vya Serikali kuwa
uteuzi kwenye vyuo hivyo unasubiri mwongozo wa Serikali na hivyo
watafahamishwa punde uteuzi utakapokamilika. Waombaji wa vyuo hivi
wanashauriwa kusubiri na kutokubadili machaguo yao hadi kutangazwa kwa
uteuzi kwa vyuo vya Ualimu vya Serikali.
Baraza pia linapenda kuwataarifu
waombaji waliokwisha chaguliwa kwenye awamu ya kwanza na wanataka kuomba
uhamisho kutoka kozi ama chuo kimoja kwenda kingine wavute subira
utaratibu utatolewa mara tu majibu ya waombaji wa awamu ya pili
yatakapotolewa.
Aidha Baraza linapenda kuwafahamisha waombaji wa Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree)
waliofanya maombi kupitia mfumo wa pamoja wa udahili wa Baraza kuwa
utaratibu wa kukamilisha maombi yao utatolewa baada ya mashauriano kati
ya Baraza na Tume ya Vyuo Vikuu yatakapokamilika.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
Tarehe: 08th Agosti, 2016
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!