Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Agosti, 2016 amemteua Bw. Andrew
Wilson Massawe kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho
vya Taifa (NIDA).
Kabla ya uteuzi huo Bw. Andrew Wilson Massawe alikuwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta katika Benki Kuu Tanzania (BOT).
Bw.
Andrew Wilson Massawe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Modestus
Francis Kipilimba ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya
Usalama wa Taifa.
Uteuzi wa Bw. Andrew Wilson Massawe unaanza mara moja.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
25 Agosti, 2016
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!