Serikali ya Tanzania imetangaza
kuzisimamisha kwa muda stesheni mbili za redio ,radio 5 na Magic FM kwa
madai ya kumtusi rais Magufuli na kuchochea ghasia nchini.
Mapema mwezi huu ,serikali pia ilipiga marufuku gazeti moja kwa kuchapisha 'habari za uongo'.
Waziri
wa mawasiliano Nape Nnauye amesema ameagiza kamati ya maadili
kuzichunguza idhaa hizo na kupendekeza hatua zaidi kuchukuliwa dhidi
yake.
Marufuku ya steheni hizo mbili inajiri huku hali ya wasiwasi
ikitanda nchini humo kufuatia hatua ya upinzani kufanya mikutano yake
nchi nzima.
Kulingana na muungano wa upinzani nchini humo
CHADEMA,mikutano hiyo kwa jina UKUTA ,inalenga kupinga kuidhinishwa kwa
sheria ya uhalifu wa mitandaoni inayokandamiza uhuru wa kujieleza
,kufutwa kazi kwa wafanyikazi wa serikali kiholela pamoja na marufuku ya
mikutano ya kisiasa ya upinzani.
Ubalozi wa Marekani mjini Dar es
Salaam umetoa ushauri wa kusafiri kwa raia wake ukiwaonya kutozuru
maeneo ambayo mikutano hiyo itafanyika.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!