Rubi ni Pasua Kichwa, ana Dharau, Anajisikia- Asema Msanii wa THT:;

Kwa mujibu wa msanii wa THT, Max Spesho ambaye ni muigizaji wa tamthilia
ya Kelele ya Clouds TV, Ruby ni pasua kichwa, ana dharau, anajisikia na
mgumu kufanya naye kazi.
Max amejitokeza kusema hayo baada ya Ruby kutangaza kujitoa kwenda
kutumbuiza kwenye Fiesta Mwanza licha ya kusaini mkataba wiki chache
zilizopita. Ruby ameitupia lawama Clouds na management ya THT kuwa
hawathamini wasanii.
Lakini Max anadai kuwa kwa wasiomjua Ruby wanaweza kuhisi anaonewa lakini wanaomjua wanafahamu alivyo na matatizo.
“Ruby ni msichana ambaye hawezi kuishi na watu wote vizuri kutokana na
the way anavyojiweka yaani mtu fulani hivi wa ususa susa na kukera kera,
vitu ambavyo watu wengi hawapendi kufanyiwa kibinadamu japo ana uwezo
mkubwa wa kuimba,” Max ameiambia Bongo5.
“Na kwa upande mwingne tunasema bado hajakuwa kiujumla,” anasema Max.
“Kwa sababu inasikitisha sana ..mama yako alokulea ukaanza kumtukana, si
utapata laana? Hata kama kakukosea waswahili wanasema mama ni mama tu
hata awe chizi atabakia kuwa mama. Uamuzi aliochukua anaweza akaona
amefanya kitu poa lakini nina uhakika amefanya kitu ambacho atakuja
kujuta maisha yake yote,” amesisitiza.
“No way out…jiulize wasanii wangapi wapo Clouds wasanii wangapi wapo THT
na ushawahi kusikia wanalamika eti pesa ndogo wanayolipwa kwenye show
au kaz yoyote! Mimi nIpo pale THT inaenda 1 year and a half sasa,
sijaona mtu akidhulumiwa,sana labda utachelewa kulipwa tu.”
“Tukienda mbali Ruby amekuwa akitukosea hadi sisi wasanii wenzie,
imagine tuko wote kituo kimoja halafu hatuongeleshani, huongei na
wenzio, bingwa wa kushushua wasanii wenzio kutukana yaan she is out of
discipline na kibaya zaidi anasahau kuwa mabosi walikuwa wakimfichia
machafu yake anayoyafanya ilimradi tu brand yake iendelee kukua.
Anatukosea wala haadhibiwi, nafikiri ndio amejisahau na kujiona kuwa
hakuna kama yeye sababu anajua kuimba na vile show zote alikuwa hakosi
basi ndio akajihakikishia hivyo na kujikuta na yeye commando. Huwezi
kujicompare na commando [Lady Jaydee] she is a legend, hayo ni mambo ya
wakubwa yaan Ruby ni worst,” amesisitiza Max.
“Niulize kitu, unaweza ukasaini mkataba kabisa wa show halafu imebakia
masaa show ifanyike ndio unasema eti huwez kufanya show maslahi maduchu?
Sasa ulisaini ili iweje? Hukusoma pale pale mkataba ulipopewa? Mazoezi
yote kafanya ya show na kwenye social anaandika kabisa kwamba yuko
excited na kuchukuliwa Fiesta na kusaini, few hours before unazngua!
Mimi nafikiri cha kumshauri Ruby kwa sasa angerudi tu kanisani aendelee
na nyimbo za dini, atapata vihela huko maana na kanisani kwenyewe nako
pia alichafua akapewa laana ya kanisani.”
Bongo5
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!