Mshambuliaji nyota na nahodha wa
Uingereza Wayne Rooney anatarajia kustaafu soka la kimataifa baada ya
kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 itakayofanyika
nchini Urusi.
Nyota huyo wa Manchester United alikuwa akizungumza
na wanahabari kwa mara ya kwanza toka kocha mpya wa timu ya taifa ya
Uingereza sam Allardyce athibitishe kuwa ataendelea kuwa nahodha.
Akihojiwa Rooney ambaye amefunga mabao 53 katika mechi 115 kwa
Uingereza, amesema pindi Kombe la Dunia la Urusi litakapomalizika
anadhani wakati wake wa kuaga soka la kimataifa utakuwa umefika.
Nyota huyo aliendelea kudai kuwa michuano hiyo itakuwa nafasi yake ya
mwisho kufanya kila kitu na Uingereza hivyo bado ataendelea kufurahia
miaka miwili iliyobakia.
Kama Rooney akicheza mchezo wa Jumapili
hii wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Slovakia, atakuwa amevunja rekodi
ya David Beckham ya kucheza mechi nyingi katika timu ya taifa.
COMMENT AND SHARE................................................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!