Wanariadha wakimbizi kutoka kote
duniani wamekuwa wakifanya mazoezi kwa bidii, lengo kuu, kushiriki
katika michezo ya Olympic chini ya bendera ya kamati ya kimataifa ya
Olimpiki.
Katika viungani mwa jiji la Nairobi, ni wakfu wa Tegla
Loroupe, ambao unasimamia mazoezi ya wanariadha watano kati ya kumi
waliochaguliwa kushiriki Michezo ya Olmpiki kule Rio de Janeiro, Brazil.
Tegla
Lorupe, anashikilia rekodi kadhaa za mbio duniani na alikuwa mwanamke
wa kwamza kutoka Afrika kushinda mbio za nyika za New York City,
alianzisha wakfu huu na nia za kuinua talanta kutoka maeneo ambayo
yanakumbwa na vita na dhamira ya kudumisha amani.
Alifanikiwa
kuzuru kambi za wakimbizi kaskazini mwa kenya na kuweza kutambua
wasichana kwa wanaume ambao wanaweza kukimbia, aliwaleta Nairobi na
kuwapea wakufunzi wa kuhakikisha kwamba wamejiandaa vilivyo.
Mbona
msukumo huu, Tegla anasema, "kama mwanariadha, nilifahamu kwamba kuna
mengi ambayo ninaweza kufanya kando na kushiriki mashindano Ulaya na
kuishi vizuri.
watu ambao wamefaulu huwa wanasahau nyumbani, lakini mimi sikusahau
nyumbani, nilirudi na kuanza mashindano ya kuleta amani na mimi kuwaona
hawa wanariadha wakienda Rio kwa ajili ya amani ninafurahia"
Mmoja
wa wale ambao walifuzu ni Angelina Naidai. Ni mkimbizi kutoka Sudan
Kusini mwenye umri wa miaka 22, alitoroka vita kutoka Sudan kusini akiwa
na miaka minane tu, na hajawahi kuona familia yake tena.
Wazo la kuwahi kuona familia yake ndilo linampa msukumo, anasema.
"Nitakapoenda,
lazima nirudi kama mtu wa maana, mtu tofauti, ndiposa niweze kuenda
kutafuta familia yangu, kwa sasa hata siwajui, siwezi kuwatambua hata,
labda wanafananishe na jamii yangu ambao nafanana nao".
Na kwa wale ambao hawakufaulu, wamepata kuona nuru katika maisha ya baadaye ya kukombolewa katika minyororo ya ukimbizi.
Riek Thiep, mwenye Umri wa miaka 24, pia ni mkimbizi kutoka sudan
kusini, alishuhudia mauaji ya mama na dada yake, na kutoroka sudan
Kusini, alijipata katika kambi ya waimbizi ya Kakuma kaskazini mwa
Kenya, na akajitahidi hadi hapa Nairobi na lengo la Kuwa bingwa siku
moja.
"Siku moja, wakati mmoja, nitakua mtu wa maana, olimpiki za
2012, raia wa Uganda alishinda medali ya dhahabu, alinifurahisha sana
hasa alayokuwa akizumgumza, alisema ata akifa yeye ni Bingwa, kwa hiyvo
siku moja watu watasema alikuwa bingwa wa medali ya dhahabu katika
Olimpiki,” anasema.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!