Rio 2016: Usain ashinda dhahabu ya mita mia 100 akifuatwa na Justin Gatlin:;
Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt,
ameandikisha historia ya kuwa mwanariadha wa kwanza kushinda nishani ya
dhahabu kwa mara ya tatu mfululizo, katika mbio za mita mia moja,
kwenye michezo ya olimpiki ya Rio 2016.
Bolt, 29, amechukua muda
wa sekunde 9.81 katika fainali yake ya mwisho katika michezo ya
olimpiki, kwa kuiga ushindi sawa na huo katika michezo ya olimpiki mjini
Beijing 2008, na London 2012.
Gatlin, ambaye amepigwa marufuku
mara mbili kwa matumizi ya dawa za kutitimua misuli, alimaliza sekunde
0.08 nyumna ya Bolt na kuchukua nishani ya fedha.
"Nilitarajia kwenda kasi zaidi, lakini nafurahia kwamba nimeshinda," Bolt ameiambia BBC.
Mwanariadha
wa Canada Andre de Grasse ameshinda nishani ya shaba, na kuandikisha
muda bora wa kibinafsi wa sekunde 9.91, mbele ya mwanariadha wa Jamaica
Yohan Blake.
Bolt anatazamia kuondoka Rio na nishani zaidi za
dhahabu katika mbio za mita 200 na mita 100 kupokezana vijiti, jinsi
ilivyokuwa katika michezo ya olimpiki ya mwaka 2008 na 2012.
Mwanariadha
huyo anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 100 alisema kuwa
atastaafu kutoka kwenye ulingo wa riadha baada ya michuano ya ubingwa
dunia mwaka 2017.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!