|
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Leicester City wamemuongezea mkataba wa miaka minne kocha wao Claudio Ranieri.
Mkataba huo mpya utamuweka kocha huyo raia wa Italia, mwenye umri wa miaka 64, kwa mabingwa hao mpaka mwezi Juni, mwaka 2020.
Ranieri anaungana na wachezaji Kasper Schmeichel, Wes Morgan na Jamie Vardy waliongeza mikataba ya muda mrefu katika klabu hiyo.
Makamu
mwenyekiti wa timu hiyo Aiyawatt Srivaddhanaprabha, amesema kocha huyo
yuko katika mpango wa muda mrefu wa timu hiyo kwa kuwa na ujuzi mkubwa
na uzoefu.
Katika msimu wake wa kwanza kocha huyo aliwapa ubingwa
timu hiyo Ranieri amewahi kuvifundisha vilabu vikubwa kama Chelsea,
Juventus, Inter Milan na AS Roma. |
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!