SAKATA la kudakwa kwa viongozi wa Simba na Taasisi ya Kupambana na
Kuzuia Rushwa (Takukuru), limechukua sura mpya baada ya viongozi wa
klabu hiyo kuanza kushikana uchawi, huku Rage akimpa siku saba Zakaria
Hans Pope kumuomba radhi.
Rage amevunja ukimya na kutaka kuombwa radhi kufuatia kauli ya
Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Usajili ya Simba, kudai kuwa fedha za
mshambuliaji Mbwana Samatta aliyeuzwa TP Mazembe zilipitia kwenye
akaunti ya mke wa Rage wakati akiwa Mwenyekiti wa klabu hiyo.
"Nadhani mtu mwendawazimu tu anaweza kufanya hivyo, mke wangu hana
hata akaunti…Kama anajua akaunti ya mke wangu aipeleke Takukuru aje
achukuliwe, mimi mtu makini, nimeshaongea na wakili wangu amshughulikie
akishindwa kuniomba radhi ndani ya siku saba. La sivyo suala hili
litaenda mahakamani," alisema Rage.
"Waache kuweweseka kinachozungumzwa ni fedha za Okwi sio fedha za
Samatta, suala hili kwa sasa lipo kwenye vyombo vya sheria, waachie
vifanye kazi yao kwani mpaka sasa ni tuhuma tu, hata wakipelekwa
mahakamani bado itakuwa ni tuhuma na wakae wakijua hii ni Awamu ya Rais
wa Tano, haina msalie Mtume, ni kumbakumba tu, ” alisema Rage.
Kauli ya Rage imekuja baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya
Simba, Zakaria Hans Pope kudai kuwa Rage ameshikia bango suala hilo
wakati yeye fedha za Samatta zilipita kwenye akaunti ya mke wake.
“Rage anapiga kelele sana pesa za Okwi yeye za Samatta zilipitia
kwenye akaunti ya mkewe na hakupigiwa kelele, “alisema Pope na kuongeza:
“Kuhamisha pesa sio kosa la jinai akaunti ilifungiwa huwezi kutumia
pesa yoyote hata kama kodi ni kidogo ya kilichopo. Kipindi hicho
hapakuwa na kodi yoyote inayodaiwa kwa hiyo hapakuwa na kosa lolote.”
“Hizi ni fitina tu kwa nini itumike Takukuru?” alihoji Pope. Takukuru
ilimshikilia Aveva kwa tuhuma za utakatishaji fedha zilizolipwa na
Etoile du Sahel ya Tunisia za malipo ya mauzo ya Mganda Emmanuel Okwi
ambaye zililipwa kwenye akaunti ya klabu ya Simba mwezi Machi mwaka huu
na uchepushaji wa fedha kutoka kwenye akaunti hiyo ya Wekundu wa
Msimbazi ndipo ulipoanzia.
Taasisi hiyo bado inaendelea na uchunguzi wa miamala ya kifedha
kwenye akaunti za viongozi mbalimbali wa Simba ikiwemo akaunti binafsi
ya Rais huyo wa Wekundu wa Msimbazi kwa kile walichodai kuwa kuna
miamala ya kutia shaka ikiwemo dola 62,000 zilizolipwa kwenye Benki ya
Hong Kong na dola 19,000, ambazo zilifanya malipo mbali mbali kwenye
akaunti za watu binafsi.
Katika mkutano huo uliofanyika hivi karibuni uliwasilisha bajeti
kivuli ya mwaka 2016/2017 ukitaka wajumbe ambao ni wanachama kuipitisha
bajeti hiyo, kitendo ambacho kiliwachefua wanachama ambao hawakuijadili
bajeti hiyo na badala yake walipiga kelele za mabadiliko na kutaka timu
akabidhiwe mfanyabiashara Mohamed Dewji maarufu ‘Mo’.
Akizungumza la kuwachomea utambi Rage alisema “nilizishikia bango kwa
vile nilishutumiwa sana kuwa mimi zile hela nimekula wakati haikuwa
hivyo, walinitia doa sana sasa wanaumbuka”.
Simba ilikuwa inaidai Etoile dola 300,000 sawa na Sh milioni 600,
lakini pia imelipwa dola 19,000 kama fidia ya usumbufu wa kufuatilia
deni hilo.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!